Alhamisi 25 Juni 2026 - 10:25
Majlisi za Imam Hussein (as) Zaendelea Kuadhimishwa kwa Hamasa Kubwa Mjini Moshi, Tanzania

Hawza/ Katika mwendelezo wa maadhimisho ya mwezi wa Muharram na kumbukumbu ya shahada ya Imam Hussein (as), majlisi za maombolezo zimeendelea kufanyika kwa hamasa kubwa katika mji wa Moshi, nchini Tanzania, huku waumini wakijitokeza kwa wingi kushiriki katika vikao hivyo vya kuhuisha ujumbe wa Karbala na maadili ya Ahlul-Bayt (as).

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Msikiti wa Ahlul-Bayt mjini Moshi umeendelea kuwa miongoni mwa vituo muhimu vya maadhimisho hayo mwaka huu, ambapo waumini kutoka maeneo mbalimbali wamekuwa wakikusanyika kwa ajili ya kushiriki katika majlisi za maombolezo ya Imam Hussein (as), mjukuu wa Mtume Muhammad (saww), aliyeuawa kwa dhuluma katika ardhi ya Karbala.

Majlisi hizo zimekuwa zikifanyika katika mazingira yaliyojaa huzuni, tafakuri na mapenzi kwa Ahlul-Bayt (as), huku washiriki wakipata fursa ya kusikiliza darsa na mawaidha mbalimbali yanayoelezea matukio ya kusikitisha yaliyotokea Karbala pamoja na malengo matukufu ya harakati ya Imam Hussein (as) ya kutetea haki, uadilifu na dini ya Kiislamu.

Wahadhiri katika majlisi hizo wameendelea kufafanua kwa kina historia ya Ashura, kujitolea kwa Imam Hussein (as) na wafuasi wake, pamoja na nafasi ya tukio la Karbala katika kuhuisha roho ya mapambano dhidi ya dhuluma na ufisadi katika jamii.

Waumini waliohudhuria wameeleza kuwa; majlisi za Imam Hussein (as) ni chuo cha maadili na mwamko wa Kiislamu kinachowakumbusha Waislamu umuhimu wa kusimama upande wa haki na kutetea misingi ya dini hata katika mazingira magumu.

Maadhimisho hayo yanaendelea katika mji wa Moshi na maeneo mengine mbalimbali nchini Tanzania, huku sauti za maombolezo, dua na mawaidha zikizidi kuhuisha kumbukumbu ya shahada ya Sayyid al-Shuhadaa Imam Hussein (as) na mashujaa wa Karbala katika nyoyo za waumini.

Majlisi za Imam Hussein (as) Zaendelea Kuadhimishwa kwa Hamasa Kubwa Mjini Moshi, Tanzania

Majlisi za Imam Hussein (as) Zaendelea Kuadhimishwa kwa Hamasa Kubwa Mjini Moshi, Tanzania

Majlisi za Imam Hussein (as) Zaendelea Kuadhimishwa kwa Hamasa Kubwa Mjini Moshi, Tanzania

Majlisi za Imam Hussein (as) Zaendelea Kuadhimishwa kwa Hamasa Kubwa Mjini Moshi, Tanzania

Majlisi za Imam Hussein (as) Zaendelea Kuadhimishwa kwa Hamasa Kubwa Mjini Moshi, Tanzania

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha