Kwa mujibu wa ripoti ya Kitengo cha tarjuma cha Shirika la Habari la Hawza, Mkusanyiko wa Wanazuoni wa Kiislamu wa Lebanon umetoa taarifa kutokana na mnasaba wa makubaliano yaliyofikiwa kati ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Marekani.
Matini ya taarifa hiyo ni kama ifuatavyo:
Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imethibitisha kwamba ni dola yenye nguvu iliyoweza kuvuka migogoro yote iliyosababishwa na uchokozi wa Kizayuni na Kimarekani uliowekewa; uchokozi ambao ulisababisha kuuawa kishahidi viongozi wakubwa akiwemo Imam Shahidi, Ayatullah al-Udhma Sayyid Ali Khamenei, na pia ulijumuisha mashambulizi makubwa ya mabomu yaliyolenga miundombinu ya kijeshi na isiyo ya kijeshi katika maeneo mbalimbali ya Iran. Iran imetoka katika vita hivi ikiwa mshindi na hatimaye imemlazimisha Marekani kukubali na kutekeleza masharti yake katika makubaliano ambayo yanatarajiwa kutiwa saini nchini Uswisi ndani ya siku chache zijazo.
Taarifa hiyo iliongeza kuwa; Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ilisisitiza kwamba makubaliano na Marekani yajumuishe pia usitishaji wa mapigano nchini Lebanon, jambo ambalo limetajwa mara tatu katika makubaliano hayo. Hili linaonesha ukweli wa Iran katika kutekeleza ahadi zake, na pia linaonyesha kwamba Iran ni rafiki wa kweli wa Lebanon, hatua hii imeimarisha mamlaka ya Lebanon; kwa sababu hiyo, maelezo ya mwisho ya makubaliano yameachiwa Walebanon wenyewe ili wafanye mazungumzo katika mazingira ya usitishaji vita, si chini ya vitisho vya vita.
Kwa hivyo, Walebanon wanapaswa kushikamana na haki zao zote kamili, ikiwemo kuyaondoa kikamilifu majeshi ya uvamizi, kusitishwa kwa mashambulizi yote, kurejea kwa wakimbizi, kuachiliwa wafungwa na kufanyika kwa ujenzi upya. Kinachoonyesha ushindi wa Iran kupitia makubaliano haya ni vilio na maombolezo yanayosikika ndani ya utawala wa Kizayuni, pamoja na ukweli kwamba Marekani imewaacha peke yao, na kwamba Muqawama na Iran ndio walioshinda katika vita hivi.
Mkusanyiko huo umeeleza: Sisi katika Mkusanyiko wa Wanazuoni wa Kiislamu, baada ya ushindi huu wa wazi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Mhimili wa Muqawama, hususan nchini Lebanon, tunatangaza yafuatayo:
Kwanza: Mkusanyiko wa Wanazuoni wa Kiislamu unatoa kiwango cha juu kabisa cha shukrani na pongezi zake kwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, kwa Walii wa Waislamu Hadhrat Ayatullah Sayyid Mujtaba Khamenei, Rais Masoud Pezeshkian, Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC), na wote waliokuwa na mchango katika kufanikisha makubaliano haya.
Pili: Mkusanyiko wa Wanazuoni wa Kiislamu unaushukuru Muqawama wa Kiislamu kwa kusimama kwake kishujaa mbele ya uchokozi wa Kizayuni, na unaona ushindi huu kuwa ni matunda ya jihadi ya mashahidi, majeruhi na wapiganaji wa njia ya Mwenyezi Mungu, ambao baada ya Mwenyezi Mungu, fadhila ya ushindi huu inarejea kwao.
Tatu: Mkusanyiko wa Wanazuoni wa Kiislamu unaitaka tena Serikali ya Lebanon kutumia fursa hii kurekebisha makosa iliyoyafanya; miongoni mwa hayo ni kurekebisha uhusiano wake na Iran, kusitisha mazungumzo ya moja kwa moja na kurejea katika mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja, pamoja na kusisitiza kusimamishwa kabisa kwa mapigano na kutekelezwa kwa vipengele vitano vya makubaliano.
Nne: Mkusanyiko wa Wanazuoni wa Kiislamu unaitaka Serikali ya Lebanon kuunga mkono mazungumzo ya kitaifa kati yake na nguvu mbalimbali za kisiasa ili kufikia msimamo mmoja wa kitaifa; msimamo unaosisitiza ufanisi wa “Mlingano wa Dhahabu” wa Jeshi, Wananchi na Muqawama.
Tano: Mkusanyiko wa Wanazuoni wa Kiislamu unautaka Muqawama wa Kiislamu kuendelea kuwa katika hali ya tahadhari kamili na kubaki tayari kwa mapambano, na kutomruhusu adui wa Kizayuni kutumia kipindi cha usitishaji vita kwa ajili ya kusonga mbele kijeshi badala ya kujiondoa, wala kutoruhusu hali kurejea katika mazingira yaliyokuwepo kabla ya tarehe 2 Machi.
Maoni yako