Kwa mujibu wa ripoti ya Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Hujjatul-Islam Sheikh Ahmad Qabalan, Mufti Mkuu wa Ja'faria na mwanazuoni mashuhuri wa Lebanon, alitoa ujumbe uliomlenga Rais wa Lebanon Jenerali Joseph Aoun, pamoja na nguvu za kisiasa za Lebanon.
Katika ujumbe huo alisema: “Kinachotokea leo kinairudisha mamlaka ya Lebanon mikononi mwa wale walioigeuza kuwa mtaji wa kisiasa na zawadi ya kiusalama katika mikono ya Washington na Tel Aviv. Katika muktadha huu, vita vya Iran dhidi ya Israel gaidi ni vita vya Lebanon pia, na asili ya malengo yake imo ndani ya maslahi ya kitaifa ya Lebanon, sisi tuko pamoja na vita hivi na ni washiriki ndani yake, yeyote anayepinga ukweli huu wa kitaifa ameisaliti nchi yake, na hakuna usaliti mkubwa zaidi kuliko usaliti wa mamlaka ya aibu ambayo imeiweka Lebanon mezani mwa Washington na Wszayuni kama zawadi.”
Aliongeza kuws: “Baadhi ya watu wanapaswa kuamka kabla hawajachelewa; kwa sababu haitutoi Lebanon kwa Wazayuni, mawakala wao na makelele yao ya vyombo vya habari, tuliuambia utawala ambao una hamu ya kuuza uhuru wa Lebanon kwamba; dunia ni dunia ya muungano, na muungano hujengwa juu ya misingi inayofanana ya kitaifa, Lebanon haiwezi kusimama isipokuwa kwa kutegemea miungano ambayo ni dhamana ya mamlaka yake mbele ya jeuri ya Israel; Israel ambayo inataka kuimeza kabisa Lebanon.”
Sheikh Ahmad Qabalan aliendelea kusema: “Utawala wa sasa na chaguo zake unaishughulikia Lebanon kama mawindo ya bure ndani ya mchezo mchafu wa vita vya uwakala, Iran ni nchi kubwa na mwaminifu sana kwa mamlaka ya kitaifa ya Lebanon, ilhali Marekani ni janga la kimataifa na adui mkubwa wa Lebanon na mamlaka yake, timu ya kisiasa inayofungamana na Marekani inapaswa kuzuiwa kuendelea na mchezo wa usaliti wa kitaifa na kisiasa; kwa sababu aliyeisaliti amana ya taifa hastahili kuaminiwa, kupitia mlinganyo huu wa mamlaka uliowekwa na Iran, imekuwa wazi kwa ulimwengu kwamba; mamlaka ya Lebanon — si Beirut pekee — ni mstari mwekundu kwa Iran; na hayo yanatokea wakati utawala wa sasa umevutiwa na mradi wa kuifanya Lebanon kuwa ya Kizayuni.”
Mufti wa Kijafari wa Lebanon aliendelea katika ujumbe wake kwa kusema: “Kwa hiyo nasema kwamba; ofisi ya Netanyahu inasema kuwa Donald Trump, Rais wa Marekani, anaunga mkono mashambulizi dhidi ya Beirut; hata hivyo baadhi ya watu bado wana kiburi, wanacheza kamari, wanachezea moto wa amani ya ndani, na wanaonyesha uadui kwa Muqawama na Iran kana kwamba Lebanon ni mali binafsi ya mtu fulani. Dhana hiyo haitatimia kwa yeyote katika nchi hii, kwa sababu Lebanon ni ushirikiano wa kitaifa wa wote.”
Alisisitiza: “Yeyote anayefikiri kwamba Israel gaidi inamfaa, basi aende huko na aiache Lebanon kwa watu wake na kwa wale waliotoa kafara za kitaifa kwa ajili yake. Ardhi na medani za kitaifa zitaukataa utawala huu wakisaliti, na kila hatua kuelekea kuifanya Lebanon kuwa ya Kizayuni itaitumbukiza nchi hii katika moto.”
Mwishoni, Sheikh Ahmad Qabalan alisisitiza kuwa: “Kwa msisitizo mkubwa tunasema kwamba; mazungumzo ya kitaifa yameanzia Ayn al-Tineh (makao ya Spika wa Bunge) na yataishia hapo hapo, na yeyote anayepuuza Ayn al-Tineh, kwa hakika ameipuuza Lebanon yenyewe.”
Maoni yako