Kwa mujibu wa Kitengo cha tarjuma cha Shirika la Habari la Hawza, harakati ya “Hamas” imepongeza majibu ya Iran na Yemen dhidi ya utawala wa Kizayuni na uhalifu wake.
Katika taarifa iliyotolewa siku ya Jumatatu, Hamas ilisema kwamba; katika kivuli cha uhalifu wa adui na mashambulizi yake yanayoendelea dhidi ya wananchi wa Palestina huko Gaza, Ukingo wa Magharibi na Quds, kwa pamoja na dhidi ya wananchi wa Lebanon, juhudi za kusitisha mashambulizi hayo na uhalifu wake unaoendelea zimekuwa jambo la dharura lenye kipaumbele.
Harakati hiyo iliongeza kuwa; mashambulizi ya Israel yanahitaji mshikamano wa pande mbalimbali katika eneo na duniani kwa ajili ya kuyakomesha, kwa sababu imekuwa wazi kwamba; utawala wa Kizayuni na mwenendo wake wa mashambulizi usio na mipaka ndio chanzo cha mvutano wote katika eneo na matokeo yake hatari katika medani ya kimataifa.
Harakati ya Hamas ilieleza kwamba; adui wa Kizayuni, kupitia mashambulizi yake yanayoendelea dhidi ya Ghaza, Lebanon na Iran, pamoja na usaliti wake na kujitoa mara kwa mara katika kutekeleza ahadi zake na kuvunja makubaliano iliyotia saini, imethibitisha kwamba; ni utawala usioheshimu ahadi wala kushikamana na makubaliano yoyote.
Harakati hiyo ilisema kuwa; vikosi vya adui vinaendelea na ukiukaji na mashambulizi yao dhidi ya makubaliano na ahadi zote za kimataifa, jambo linalothibitisha kwamba sera za kivamizi za utawala wa uvamizi ni tishio la kudumu kwa usalama na uthabiti wa eneo.
Hamas katika taarifa yake ilisisitiza kwamba; mashambulizi ya Israel dhidi ya Ghaza, Lebanon na Iran hayalengi tu pande hizo, bali ni mashambulizi dhidi ya Umma mzima wa Kiislamu na uwezo wake.
Harakati hiyo ilisisitiza kwamba; jambo hili linazilazimisha sehemu zote za Umma kusimama kwa pamoja dhidi ya mashambulizi haya yanayoendelea na kuimarisha aina zote za mshikamano na uungaji mkono ili kusaidia kuzuia uvamizi wa utawala wa Kizayuni na kudhibiti ongezeko la mashambulizi yake.
Inafaa kutajwa kwamba; Vikosi vya Jeshi la Yemen siku ya Jumatatu vilitangaza kutekeleza operesheni ya kijeshi dhidi ya malengo nyeti yanayohusishwa na utawala wa Kizayuni katika eneo la Yafa, na kusisitiza kwamba; operesheni hiyo ilifanywa kwa kutumia kundi la makombora na ilifikia malengo yake kwa usahihi.
Vikosi hivyo katika taarifa yao ya leo asubuhi vilitangaza kupiga marufuku usafiri wowote wa majini unaohusishwa na adui wa Kizayuni katika Bahari Nyekundu, na vikazingatia harakati zozote za Kizayuni ndani ya eneo la operesheni zao za kijeshi kuwa ni malengo yanayoweza kushambuliwa na vikosi vyao.
Vikosi hivyo vilibainisha kwamba; operesheni za kijeshi zitaendelea kwa kiwango kinachoongezeka, na kusisitiza kwamba vitajibu hatua yoyote ya kuongeza mvutano kwa hatua kama hiyo, na kwamba harakati zao za kijeshi zitaenda sambamba na maendeleo ya makabiliano yanayoendelea.
Wakati huo huo, Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu la Iran lilitangaza kutekeleza operesheni kubwa ya kijeshi ndani ya maeneo ya utawala huo, na kuongeza kwamba; Kikosi cha Anga za Juu cha Jeshi hilo kilishambulia maeneo ya adui kwa makombora ya balestiki, makombora ya cruise na ndege zisizo na rubani za kisasa, na kuilenga Tel Aviv, viunga vyake, kusini mwa Israel, Jangwa la Naqab pamoja na makao makuu ya kijasusi na operesheni katikati ya utawala huo.
Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu lilisisitiza kwamba; mashambulizi dhidi ya Tel Aviv yalikuwa ni majibu kwa jeuri ya utawala wa Kizayuni na mashambulizi yake ya wazi dhidi ya mamlaka ya nchi ya Iran kupitia kushambulia miji na ardhi zetu, na yalikuwa katika kutimiza ahadi zetu za kuilinda nchi na damu za mashahidi.
Maoni yako