Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, hafla hiyo ilishuhudia mkusanyiko mkubwa wa waumini wa madhehebu mbalimbali, hususan Shia na Sunni, ambapo washiriki walipata fursa ya kusikiliza mawaidha na nasaha zilizolenga kuimarisha uelewa kuhusu nafasi na umuhimu wa tukio la Ghadeer katika historia ya Uislamu. Mazingira ya hafla hiyo yalitawaliwa na hali ya upendo, udugu na mshikamano miongoni mwa waliohudhuria.
Katika hafla hiyo, wazungumzaji mbalimbali walipanda jukwaani na kutoa maelezo ya kina kuhusu tukio la Ghadeer Khum, huku wakibainisha nafasi yake katika historia ya Kiislamu pamoja na mafunzo yanayoweza kupatikana kutokana na tukio hilo. Aidha, walisisitiza umuhimu wa Waislamu kushikamana na maadili ya dini pamoja na kudumisha umoja na kuheshimiana licha ya tofauti za kimadhehebu.
Miongoni mwa wazungumzaji waliohutubia katika hafla hiyo alikuwa Sheikh Ramadhani Nsweme, ambaye alitoa nasaha na maelezo ya kina kuhusu tukio la Ghadeer, huku akielezea nafasi yake katika historia ya Uislamu na umuhimu wa kulitafakari kwa mtazamo wa kielimu, upendo na kuimarisha mshikamano wa Waislamu.
Washiriki wa hafla hiyo pia walionesha kufurahishwa kwao na namna programu hiyo ilivyofanikiwa, huku wakisisitiza umuhimu wa kuendelea kufanyika kwa matukio ya aina hiyo ambayo huimarisha elimu ya dini, huongeza mapenzi baina ya waumini na kutoa fursa ya kujifunza historia ya Kiislamu kwa kina zaidi.
Hafla hiyo ilihitimishwa kwa dua, psmoja na kumtakia amani Mtume Muhammad (s.a.w.w) na Ahlul-Bayt (a.s), huku washiriki wakiondoka wakiwa na furaha na hisia za kuendelea kudumisha mafundisho ya Kiislamu pamoja na mshikamano katika jamii.




Maoni yako