Jumanne 9 Juni 2026 - 13:41
Adui kupitia vita vya kisaikolojia anapima kiwango cha ustahimilivu wetu/ Majukumu ya wabebaji wa ujumbe wa dini katika kuvuka changamoto za vita mseto

Hawza/ Mjumbe wa Baraza Kuu la Hawza, huku akisisitiza nafasi ya wanafunzi wa Hawza na wanazuoni katika kusimamia uwanja wa ufafanuzi wa mambo, amewataka wawahimize watu kuwa na “ustahimilivu” na “subira yenye malengo” ili adui alazimike kurudi nyuma.

Kwa mujibu wa mwandishi wa Shirika la Habari la Hawza, Ayatullah Sayyid Muhammad Gharawi, mjumbe wa Jumuiya ya Walimu wa Hawza na Baraza Kuu la Hawza, pamoja na mkuu wa Kitengo cha Saikolojia katika Taasisi ya Utafiti ya Hawza na Chuo Kikuu, huku akifafanua vipengele vya vita mseto na mashinikizo ya kiuchumi ya adui dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, alisema:

Adui kwa uwekezaji mkubwa analenga kuunda mazingira yatakayo wafanya watu washindwe kustahamili. Mashinikizo yanayowekwa dhidi ya Iran kupitia vikwazo vya kidhalimu yameundwa kwa mkakati huo huo ili kupitia ongezeko la mfumuko wa bei na matatizo ya maisha, kuwabana wananchi.

Kilele cha uadui wa Marekani dhidi ya Wairani na vikwazo vya sasa dhidi ya Iran havijawahi kushuhudiwa duniani

Mjumbe wa Jumuiya ya Walimu wa Hawza ya Qom aliongeza: Ni lazima izingatiwe kwamba; uchumi wetu, ingawa una udhaifu fulani katika sekta ya uzalishaji na masuala ya ndani, lakini vikwazo vya sasa dhidi ya Iran havina mfano duniani, katika kipindi chochote wala kwa kiwango chochote, hakuna nchi iliyowahi kuwekwa chini ya shinikizo la aina hii.

Ni lazima ifahamike kwamba; hata nchi kubwa na madola makubwa, kama zingekabiliwa na kiwango hiki cha vikwazo vya pande zote, zingekumbana na matatizo makubwa sana ya kiuchumi, adui akitambua jambo hili, ameendelea kuongeza mashinikizo siku baada ya siku.

Ayatullah Gharawi akigusia malengo ya mwisho ya mfumo wa utawala wa kidunia alisema: Mashinikizo haya yote ni kwa ajili ya kuwafanya wananchi wawe chini ya shinikizo la kiuchumi na kupoteza uwezo wao wa kustahamili; matokeo ya kupungua kwa ustahamilivu huu ni kutokea kwa ghasia zisizoelekezwa, kuingia moja kwa moja kwa adui kupitia mipaka ya ardhini, angani na baharini, na hatimaye kugawanyika nchi au kuwafanya viongozi wajisalimishe mbele ya matakwa ya kiburi cha kimataifa.

Katika baadhi ya matukio, adui baada ya kuona baadhi ya ishara za kijani kutoka ndani ya nchi, amekuwa na matumaini makubwa zaidi kuhusu njama hii.

Mjumbe wa Baraza Kuu la Hawza za Kiislamu akirejelea matukio ya zamani alisema: Katika baadhi ya matukio yaliyopita, adui alianza kwa migomo kisha akaipanua kuelekea uharibifu na mauaji ya watu, na hapo akaonyesha uhalisia wake.

Kwa muda ambao maandamano yalikuwa katika kiwango cha kauli mbiu, yalivumilika; lakini pale adui alipolenga mauaji, uharibifu na maangamizi, vikosi vya usalama na baadaye wananchi wenyewe waliingia uwanjani na kuwazuia wachochezi — iwe wale waliodanganywa au wale waliokuwa mawakala wa adui.

Mkuu wa Kitengo cha Saikolojia katika Taasisi ya Utafiti ya Hawza na Chuo Kikuu alisema: Leo pia adui kupitia michezo ya kisaikolojia anapima kiwango chetu cha ustahimilivu, anafikiri kwamba kwa kuunda mashinikizo ya kivita, kuvuruga mauzo ya mafuta, kuzuia uingizaji wa bidhaa na kufunga mipaka ya ardhini, anaweza kutufanya tusalimu amri, lakini hesabu hizi si sahihi, kwa sababu mashinikizo haya yameundwa kwa malengo ya kiusalama ili kumwezesha kuingia nchini na kuwaua viongozi.

Ayatullah Gharawi akisisitiza umuhimu wa suala la ustahimilivu katika vita vya kulazimishwa vya siku mia moja vya hivi karibuni alisema:  Adui katika mapambano haya ilielekeza ncha ya mashambulizi yake moja kwa moja kwa uongozi na mihimili ya mfumo wa utawala; lakini kuuawa kishahidi kwa kiongozi wetu mpendwa kulikuwa na nafasi muhimu na ya kuamua katika kuliamsha taifa.

Kuuawa kishahidi yeye kulisababisha watu wengi waliokuwa katika tabaka la kati la jamii kufahamu malengo maovu ya adui ya kuigawa Iran na kuingia uwanjani.

Aliendelea kusema: Uwepo wa wananchi una majukumu mawili muhimu sana:

Kwanza: huimarisha hamasa na ari miongoni mwa watu.

Pili: huondoa hofu ambayo adui hueneza kupitia propaganda za vyombo vya habari.

Aliongeza kuwa: Mtu anapokaa nyumbani huingiwa na hofu, lakini anapotoka na kujiunga na wananchi wengine, hofu hiyo hupungua na hali ya kishujaa huitawala jamii.

Mjumbe wa Baraza Kuu la Hawza alisema mwishoni: Mafanikio ya vikosi vya kijeshi na ustahimilivu wa kipekee wa taifa kwa vitendo vimeifanya Iran kuwa nguvu kubwa na hata dola kubwa, jambo muhimu ni kwamba; watu wengi ambao kwa sababu ya propaganda za adui walikuwa wameanza kuwa na mashaka kuhusu utambulisho wao wa kitaifa na kijamii, sasa baada ya kuona msimamo dhidi ya madola makubwa, wanajivunia utambulisho wao wa kitaifa na wameelewa kwamba nchi yao imesimama kidete katika ngazi ya kimataifa juu ya misingi yake.

Ufahamu huu na ustahimilivu huu ni dhamana ya kuendelea kuwepo na nguvu ya mfumo mbele ya njama zote za maadui.

Umuhimu wa “ustahimilivu” katika kuvuka changamoto za vita mseto

Ayatullah Gharawi, akiendelea na uchambuzi wake wa hali ya sasa ya nchi Iran, alizungumzia athari ya nguvu za kijeshi na kisiasa za Jamhuri ya Kiislamu katika hali ya jumla ya jamii na akasema: Msimamo madhubuti wa Iran dhidi ya matakwa ya Marekani, kulenga vituo vyao, pamoja na udhibiti wa kimkakati wa njia muhimu za maji kama Mlango wa Hormuz, umethibitishia ulimwengu kwamba dhana za awali kuhusu uwezo wa Iran zilikuwa si sahihi.

Alisema: Leo hata wale ambao huenda zamani walikuwa na mtazamo tofauti au walishiriki katika baadhi ya mikusanyiko, baada ya kuona uimara wa mfumo katika kulinda usalama na utambulisho wa Iran wamejitokeza uwanjani, hili linaonyesha kuzaliwa kwa hisia maalumu ya utambulisho wa kitaifa miongoni mwa wananchi.

Wamegundua kwamba viongozi wa mfumo kwa uaminifu wamewekeza kwa ajili ya usalama na heshima ya nchi hii, na madai yote ya adui katika miaka hii yalikuwa si chochote isipokuwa uongo na batili.

Ayatullah Gharawi akitoa shukrani kwa juhudi za wanafunzi wa Hawza na wanazuoni alisema: Usimamizi wa nyanja hizi na wanahawza ni jambo muhimu sana kwa sababu huzuia mwelekeo kupotoka kuelekea tabia zisizo sahihi.

Aliendelea: Sasa tunakaribia mwezi wa Muharram, na wabebaji wa ujumbe wa dini wana jukumu la kueleza ukweli wa hali ya nchi na mashinikizo ya vita vya kiuchumi kwa wananchi.

Ni lazima wananchi wafahamishwe kwamba; kufikia heshima na utukufu wa vizazi vijavyo vya Iran kunategemea “ustahimilivu” na “subira yenye ufahamu” ya leo.

Ikiwa hali hii ya mapambano itaendelea, adui ambaye hataona njia nyingine isipokuwa kushindwa atalazimika kukubali maslahi ya taifa la Iran.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha