Kwa mujibu wa Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Hujjatul-Islam wal-Muslimin Sheikh Ali al-Khatib, Makamu Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Kiislamu la Mashia nchini Lebanon, alisema kwamba; taarifa iliyotolewa kutoka Washington kuhusu mazungumzo haikutushangaza, lakini jambo lililotushangaza ni kwamba serekali ya Lebanon kupitia wanadiplomasia wake ilikubali maudhui ya taarifa hii na ikakubali maelezo yake.
Alibainisha kwamba; taarifa hii inafungua milango ya fitna ya ndani ambayo daima tumekuwa tukiitahadharisha na tunaendelea kuitahadharisha; na hilii ni miongoni mwa malengo ya adui ambaye ameshindwa na ataendelea kushindwa katika kuuangamiza muqawama.
Kauli za Sheikh al-Khatib zilitolewa katika makao ya Baraza Kuu la Mashia katika eneo la Hazmieh, ambapo alianza kwa kuzungumzia tukio la Idi ya Ghadir na kumbukumbu ya mwaka wa kufariki kwa Imam Khomeini, akisema: "Shukrani zote ni za Mwenyezi Mungu ambaye ametutukuza kwa siku hii na akatuweka miongoni mwa wenye kutekeleza ahadi na mapatano yao, na shukrani ni za Mwenyezi Mungu ambaye ametufanya kuwa miongoni mwa wanaoshikamana na Wilaya ya Amirul-Muuminin na Maimamu (as)."
Hii ni dua ambayo Waumini huisema kwa ajili ya kupeana pongezi za Idi ya Ghadir; siku ambayo Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) aliitekeleza amri ya Mwenyezi Mungu kwamba:
"Ewe Mtume! Fikisha yale yaliyoteremshwa kwako kutoka kwa Mola wako, na ikiwa hutafanya hivyo basi hujafikisha ujumbe Wake..."
Aliongeza: Mtume wa Mwenyezi Mungu aliwaita mahujaji baada ya kurejea kutoka Hija ya Kuaga ili wakusanyike Ghadir Khum, na akawahutubia khutuba yake mashuhuri; khutuba ambayo baada ya kuandaa mazingira ya kutangaza uteuzi wa Imam Ali (as) kuwa kiongozi wa Waumini, alisema: "Basi angalieni namna mtakavyoshughulika baada yangu na vitu viwili vya thamani (Thaqalayn) nitakavyoviacha miongoni mwenu."
Mtu mmoja akauliza: “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Hivyo vitu viwili vya thamani ni nini?”
Akasema: "Kitu kikubwa zaidi ni Kitabu cha Mwenyezi Mungu ambacho upande mmoja wake uko mkononi mwa Mwenyezi Mungu na upande mwingine uko mikononi mwenu; basi kishikamaneni nacho ili msipotee. Na kingine ni kitu kidogo zaidi, nacho ni kizazi changu (Ahlul-Bayt wangu); na Mwenyezi Mungu amenijulisha kuwa viwili hivyo havitatengana mpaka vitakaponijia kwenye Hodhi [ya Kawthar]. Hivyo nimemuomba Mola wangu kwa ajili ya viwili hivyo; basi msivitangulie mkapotea wala msivipuuze."
Kisha akainua mkono wa Imam Ali (as) mpaka kwapa zake zikaonekana na wote wakaona, kisha akasema: "Enyi watu! Ni nani mwenye haki zaidi juu ya Waumini kuliko nafsi zao?"
Wakasema:
"Mwenyezi Mungu na Mtume Wake wanajua zaidi."
Akasema:
"Hakika Mwenyezi Mungu ni Mola wangu, na mimi ni kiongozi wa Waumini, nami nina haki zaidi juu yao kuliko nafsi zao. Basi yeyote ambaye mimi ni kiingozi wake, Ali ni kiongozi wake."
[Akarudia jambo hilo mara tatu au nne].
Kisha akasema:
"Ewe Mwenyezi Mungu! Mpende anayempenda, na umchukie anayemchukia..."
Na baadaye ukateremka Wahyi:
"Leo nimekukamilishieni dini yenu na nimetimiza neema yangu juu yenu..."
Sheikh al-Khatib aliendelea kusema: Kisha watu walimpongeza Amirul-Muuminin (as); na miongoni mwa Maswahaba, Abu Bakr na Umar walikuwa miongoni mwa waliompongeza wakisema:
"Pongezi kwako ewe mwana wa Abu Talib! Leo umekuwa kiongozi wangu na kiongozi wa kila muumin mwanamume na mwanamke..."
Alisema: Ilikuwa wazi kwamba nyuma ya uteuzi wa Imam Ali (as) kuwa kiongozi wa Waumini, Wilaya hii haikuhusiana tu na kushika dola; kwa sababu lengo si dola yenyewe, bali dola ni nyenzo ya kuilinda dini dhidi ya kupotoshwa na kuzuia dini isigeuzwe kuwa chombo cha kufikia matamanio ya watawala kwa lengo la kuufanya Umma kuwa watumwa wao.
Kwa sababu hiyo, Imam Ali (as), baada ya kuwekwa kati ya kuchagua utawala na Umma, aliuchagua Umma na akasema:
"Mimi nitaendelea kujiepusha [na vita dhidi yao] maadamu mambo ya Waislamu yatakuwa salama."
Taarifa ya Washington ni mwanzo wa fitna ya adui na kuudhuru muqawama
Makamu Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Kiislamu la Mashia nchini Lebanon, kuhusu hali ya Lebanon alisema: Taarifa yenye kuchochea fitna iliyotolewa kutokana na mazungumzo ya Jumanne na Jumatano zilizopita huko Washington haikutushangaza; lakini kilichotushangaza ni kukubali kwa utawala wa Lebanon kupitia wanadiplomasia wake, maudhui ya taarifa hiyo na kukubali hoja zake.
Je, ni jambo la kiakili kwamba taarifa hii ilitaje kundi linalopigana na adui Mzayuni anayekalia ardhi yake kuwa ni “adui wa Lebanon”?
Na huo ni mkataba wa aina gani wa kusitisha vita ambao unapuuza ukaliaji wa Kizayuni wa ardhi yetu na kuweka sharti kwamba Walebanon wajiondoe katika ardhi yao kwa manufaa ya vikosi vya uvamizi?
Anaamini kwamba: Taarifa hii, mbali na kuwa ruhusa ya wazi kwa adui Mzayuni kuendelea na vita vya mauaji ya kimbari nchini Lebanon, pia inafungua milango ya fitna ya ndani ambayo daima tumekuwa tukiitahadharisha; hili ndilo lengo ambalo adui ameshindwa kulifikia na ataendelea kushindwa katika kuuangamiza muqawama.
Sheikh al-Khatib aliongeza: Ni wazi kwamba serikali ya Marekani inaikabidhi Lebanon na kusini mwa nchi hiyo kama zawadi kwa Israel ili Israel iweze kujinusuru dhidi ya mashinikizo ya Kizayuni juu ya Washington, na pia ijiandae kwa mazungumzo magumu na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, na vilevile kuiokoa timu tawala ya utawala wa Kizayuni kutoka katika mkwamo wake ulio wazi karibu na uchaguzi.
Makamu Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Mashia aliendelea: Tulieleza katika hotuba yetu kwenye mkutano wa viongozi wa kidini Jumanne iliyopita kwamba; tunaangalia kwa tahadhari kauli ya ghafla ya [Marekani] kuhusu kusitisha vita, lakini tunataka usitishaji vita wa kina ambao utaweka mazingira ya kuondoka kikamilifu Israel kutoka katika ardhi za Lebanon, kwa namna ambayo utaruhusu kurejea kwa wakazi katika makazi yao, kuanza kwa mchakato wa ujenzi upya na kuachiwa huru wafungwa kutoka magereza ya Israel.
Ni katika hali hiyo tu ndipo inaweza kuwa na uhakika kuhusu mustakabali wa hali ya mambo.
Lakini baada ya matokeo hasi na ya kufedhehesha yaliyotoka Washington, tunaamini kwamba; ikiwa wenye maamuzi na wasimamizi wa mambo hawatarekebisha hali ya sasa, basi mustakabali wa nchi utakuwa wa hatari sana.
Kwa hiyo tunatahadharisha dhidi ya kuendelea na mkondo huu ambao hautaleta chochote isipokuwa mauaji zaidi, umwagaji damu zaidi na uharibifu zaidi.
Maoni yako