Kwa mujibu wa Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Mahakama Kuu ya Jinai nchini Bahrain imetoa hukumu nzito ya pamoja dhidi ya makumi ya raia wa Kishia, akiwemo mwanazuoni mmoja wa dini na wanawake wawili katika kesi tofauti.
Mkuu wa Mashtaka ya Uhalifu wa Kigaidi alitangaza kwamba; mahakama hiyo imewashughulikia raia watatu waliokuwa wamekamatwa kwa tuhuma zinazohusiana na kulaani mashambulizi ya Israel na Marekani dhidi ya Iran.
Vyanzo vya ndani vilieleza kwamba; hukumu za kifungo cha maisha zinawahusu watu wakiwemo: Sayyid Muhammad Hadi Hassan, Sayyid Muhammad Fadhl Hamid, Yusuf Ahmad Sarhan, Sahlan Abdulridha Mahdi, Abbas Abdullah Matar, Murtadha Hussein Awwal, mwanazuoni Sheikh Ahmad Issa Al-Haiki pamoja na mtu mwingine aliyeko nje ya nchi.
Aidha, “Ali Hussein Ali Aal Aboud” alihukumiwa kifungo cha miaka 10, huku “Sarah Abdulnabi Habib” na “Elias Salman Mirza” kila mmoja akihukumiwa kifungo cha miaka mitatu.
Matini hiyo inaeleza kwamba; hukumu hizi zinakuja katika mfumo wa kile ilichokieleza kuwa ni ajenda ya mamlaka za Bahrain ya kufungua kesi kwa kutumia tuhuma za kubuni dhidi ya raia wa Kishia.
Pia imeeleza kwamba; hatua hizo ni sehemu ya kile ilichokitaja kuwa kampeni ya kulipiza kisasi ambayo imelenga mamia ya raia baada ya kile ilichodai kuwa ni kushindwa kwa taasisi za kijeshi katika kukabiliana na Iran, kufuatia mashambulizi ya makombora ya Iran dhidi ya vituo na maslahi ya Marekani mjini Manama wakati wa vita ambavyo matini hiyo imevitaja kuwa vilianzishwa tarehe 28 Februari 2026 na Marekani pamoja na utawala wa Kizayuni kwa msaada wa baadhi ya nchi za Ghuba dhidi ya Iran.
Maoni yako