Ijumaa 29 Mei 2026 - 14:00
Israel Imeshindwa katika “Vita Vyake Vikubwa” na Hakuna Dhamana ya Kulinda Mamlaka ya Lebanon Isipokuwa Muqawama

Hawza/ Mufti Mkuu wa Kijaafari na mwanazuoni wa Kishia nchini Lebanon, akirejelea kushindwa kwa kimkakati kwa Marekani na utawala wa Kizayuni, aliongeza: Leo ni wakati wa kihistoria sana.

Kwa mujibu wa kitengo cha tarjuma cha Shirika la Habari la Hawza, Hujjatul Islam Sheikh Ahmad Qabalan, Mufti Mkuu wa Kijaafari na mwanazuoni wa Kishia nchini Lebanon, ametoa ujumbe wa Idi ya Adh-ha ya mwaka huu. Katika ujumbe huo, huku akirejelea ukweli wa “takbira ya mbinguni” ambayo ina maana ya kuiweka nafsi katika njia ya Mwenyezi Mungu na Umma mmoja mbele ya miradi ya uasi na ufisadi wa kimataifa, alisisitiza kwamba: ibada za Hija zinazotuunganisha na Mwenyezi Mungu Mtukufu haziwezi kutimia isipokuwa kwa kukataa miradi ya kuleta mifarakano, makundi ya kisiasa na ufuasi wa maangamizi kwa madola ya kiburi cha kimataifa.

Hija ina maana ya kuunganisha kwa Umma wa Kiislamu chini ya bendera ya Tawhidi; vita vya Marekani na Israel dhidi ya Iran vimeshindwa

Sheikh Ahmad Qabalan akifafanua vipengele vya kiroho na kisiasa vya Hija alisema: Hija katika mantiki ya Mwenyezi Mungu ina maana ya kujisalimisha mbele ya nguvu moja ya Kiungu kwa msingi wa mradi wa juu, ibada za Hija na taratibu za Idi ya Adh-ha ni alama ya Tawhidi na mfumo wa wajibu wa Umma mmoja pamoja na masharti ya mradi wake wa kimaarifa na wa kijamii ulio mpana, hii ndiyo maana ya “ukombozi wa mbinguni wa ardhi na mwanadamu”; kwani Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa kutangaza ibada hizi za pamoja aliikomboa ardhi na mwanadamu ili wawe ni Wake pekee.

Akirejelea hali ya sasa ya ulimwengu wa Kiislamu alisema: Leo umati mkubwa wa mahujaji wa Nyumba ya Mwenyezi Mungu wanatoa roho ya ibada hizi mbele ya Mwenyezi Mungu kama Umma mmoja bila ubaguzi wowote; lakini pamoja na hayo, serikali za nchi za Kiislamu kutokana na michezo ya kisiasa, uadui na utegemezi mbalimbali — isipokuwa chache sana — zimegawanyika, hapa ndipo lilipo janga lililoikumba sehemu kubwa ya ulimwengu wa Kiislamu; ulimwengu ambao uko karibu kugeuzwa kuwa “nyara za kifedha, kisiasa na kiuchumi” kwa Marekani, Israel na NATO.

Sheikh Qabalan akirejelea kushindwa kimkakati kwa Marekani na utawala wa Kizayuni aliongeza: Leo ni wakati wa kihistoria sana; kwa sababu vita vya Marekani na Israel dhidi ya Iran vimeshindwa vibaya sana, na uwezo wa kimkakati wa Marekani ambao ulikuwa karibu kuumeza ulimwengu, umevunjika katika vita vya Iran na Mlango Bahari wa Hormuz.

Alisisitiza: Israel ambayo Washington na NATO waliiandalia ghala la silaha kwa ukubwa wa “ramani ya Israel kubwa”, imepoteza “vita vyake vikubwa” katika makazi yote ya mipakani kwa mikono ya muqawama wa kishujaa na wenye ushindi, kwa msaada wa Mwenyezi Mungu. Ukweli wa Lebanon ya leo unatukabili na wajibu wa mshikamano wa kitaifa, mbali na miradi ya utengano inayofuatwa na baadhi ya vyombo vya mamlaka, vyombo vya habari vya fitna na baadhi ya pande zilizojaa chuki. Mfumo wa Lebanon hauwezi kuvumilia chaguo lolote la kujiangamiza, karatasi za ndani za Lebanon zina nguvu na zinafaa kwa harakati za kisiasa za kimamlaka, kwa sababu muqawama unapigana vita vikubwa zaidi vya kihistoria vya ustahimilivu na unavunja ghala hatari zaidi la Kizayuni na Kimarekani katika mstari wa mbele.

Sheikh Qabalan akisema kwamba; hakuna dhamana yoyote ya kulinda mamlaka na mipaka ya Lebanon isipokuwa muqawama wa kishujaa na wananchi wake, alifafanua: Jeshi la Lebanon katika mazingira haya kuwa ni dhamana ya amani ya ndani, na hakuna hatari kwa jeshi hilo isipokuwa kutoka katika majaribio ya mamlaka ya Lebanon na kuangukia kwake katika mradi wa Marekani na Wazayuni unaotaka kuilipua Lebanon kutoka ndani. Leo nchi ipo katika mgogoro mkubwa; kwa sababu mamlaka ya Lebanon imeacha mipaka na medani za mamlaka kwa ajili ya kuiridhisha Marekani na kurahisisha mazungumzo na Tel Aviv, hali hii wakati ambapo mafanikio ya kimamlaka ya muqawama kwa Lebanon ni makubwa zaidi kuliko yote yaliyowahi kutolewa tangu kuanzishwa kwa nchi hii.

Mamlaka ya Lebanon inaongoza mazungumzo hatari zaidi ya kujisalimisha na Israel gaidi

Aliendelea kwa kukosoa utendaji wa mamlaka ya Lebanon na kusema: Wakati muqawama unaandika mashujaa wakubwa wa kimamlaka, mamlaka ya Lebanon inaongoza mazungumzo hatari zaidi ya kujisalimisha na Israel gaidi, lazima tujihadhari na michezo ya fitna ya nje; kwani kuna watu wanaotaka kuupiga mkataba wa kitaifa na kuilipua Lebanon, hakuna kitu hatari zaidi kwa Lebanon kuliko fitna ya ndani.

Sheikh Qabalan akimuelekea Rais Joseph Aoun alisema: Unaweza kuwa rais wa kuijumuisha Lebanon yote, na sisi hatukubali uwe rais wa kuigawa, uchaguzi uko mikononi mwako, inapaswa kufahamika kwamba Lebanon ipo katika eneo linalowaka moto, na mradi wa Marekani haulitafutii mema eneo hili wala Lebanon, bali unataka kuliteketeza eneo hili baada ya kushindwa vibaya kwa hadhi ya Washington katika Mashariki ya Kati, kuikinga Lebanon huanza kwa umoja wa kitaifa, mshikamano wa kimamlaka na uelewa wa mamlaka ya Lebanon kuhusu ukweli wa mambo, itikadi, mkataba wa kitaifa na ulazima wa kulinda jeshi na amani ya ndani dhidi ya fitna za Washington na Tel Aviv.

Hakuna jambo muhimu zaidi kwa Lebanon baada ya mamlaka yake na medani zake za kitaifa kuliko umoja na amani yake ya ndani

Sheikh Ahmad Qabalan alisisitiza: Hakuna jambo muhimu zaidi kwa Lebanon baada ya mamlaka yake na medani zake za kitaifa kuliko umoja na amani yake ya ndani, na kung’ang’ania kwa baadhi ya watu kuigawa Lebanon kwa manufaa ya Washington na mipango ya Tel Aviv kunaisukuma Lebanon kulielekea janga baya zaidi, Lebanon maana yake ni ushirikiano, maelewano, mawasiliano, mshikamano na itikadi ya kitaifa; vinginevyo Lebanon itasambaratika.

Aliendelea: Muqawama kwa kujitolea kwake, historia yake na hali yake ya sasa ni dhamana kubwa zaidi kwa Lebanon, na mamlaka ya Lebanon inalazimika kutoa majibu ya kitaifa, ya mipakani na ya kuleta umoja; si kuiuza Lebanon, si kuugawa umoja wake wa ndani na si kuwasha moto katika itikadi yake ya kitaifa. Aliyeikomboa Lebanon kutoka katika ukaliaji wa Kizayuni hawezi kuukubali Uzayuni tena; na yule aliyelivunja ghala la jeshi la Kizayuni katika mstari mzima wa mbele hatavumilia kuchomwa kisu mgongoni.

Kutatua matatizo ya Lebanon kupitia mazungumzo ya aibu ya siri na Tel Aviv gaidi haiwezekani

Mwanazuoni huyo wa Kishia wa Lebanon alisisitiza: Kutatua matatizo ya Lebanon kupitia mazungumzo ya siri ya aibu na Tel Aviv gaidi haiwezekani, na kulivuta jeshi la Lebanon katika mchezo huu kutaiweka Lebanon katikati ya machafuko ya hatima, leo hakuna dhamana kwa Lebanon isipokuwa muqawama na jeshi la Lebanon, na kulishambulia jeshi la Lebanon katika mchezo wowote wa Marekani na Wazayuni kutaiwasha Lebanon moto. Mamlaka ya Lebanon pia inabeba jukumu kubwa mbele ya janga lolote litakalotishia amani ya ndani, na hapa ninamwambia kila anayehusika na maneno haya kwamba: “Rais Nabih Berri” ni utajiri wa kitaifa na uwezo wa kihistoria wa maridhiano, na akili pamoja na uelewa wake wa kitaifa ni dhamana kubwa zaidi kwa serikali, makundi ya kijamii, dhana ya mamlaka na kila kitu kinachohitajika katika suluhu za kitaifa za pamoja mbali na mchezo wa kugawa, kuleta mifarakano, kuisahilisha Lebanon na fitna za Kimarekani, bila njia yake hakuna suluhisho, na hakuna suluhisho litakalokubalika kwa gharama ya mamlaka ya kitaifa na umoja wa ndani; huku nchi sasa ikiwa katika mazingira yake magumu zaidi na yenye hatari.

Sheikh Qabalan pia alisisitiza: Vikosi na vyama vya kisiasa vina wajibu wa kuilinda Lebanon dhidi ya kamari hatari zaidi ya kisiasa, Uislamu na Ukristo ni historia ya Lebanon katika ulimwengu wa kuishi pamoja, maisha ya pamoja na familia ya kitaifa, Beirut ni pafu la Dahieh na ngome yake imara, Jabal Al-Muwahhidin Al-Druzi ni ndugu wa kihistoria wa Jabal Amil, Jabal Keserwan ni sehemu iliyoungana ya historia ya Beqaa na tambarare zake, Kusini mwa Lebanon bila kaskazini mwa Lebanon na mapenzi yake hakuna thamani yoyote; historia ni moja na kujitolea ni kule kule, hamu na mapenzi ya Walebanon ndio dhamana kubwa zaidi kwa Lebanon adhimu.

Aliendelea kusema: Watu wa kusini, Dhahieh na Beqaa ni kiini cha ukarimu, utoaji na kujitolea adimu katika ulimwengu wa mashujaa wa kitaifa, na wajibu wa kweli ni umoja wa Lebanon, ushirikiano wa familia yake ya kitaifa, kulinda mipaka na mamlaka yake pamoja na kuendeleza vita vikubwa na adhimu zaidi vya kimamlaka vinavyoongozwa na muqawama wake wa kishujaa huku jeshi likiulinda ili “Lebanon ya Uislamu, Ukristo na ushirikiano wa kitaifa” ibaki. Ikiwa kutakuwa na jambo la kutakiwa kwa maslahi ya Lebanon na eneo hili, basi hakuna jambo muhimu zaidi kuliko “makubaliano ya Saudi-Iran” kwa ajili ya kuzima mgogoro wa Lebanon na eneo hili na kudhibiti fitna za “madalali wa Washington na Tel Aviv” wanaotaka kuwasha moto katika muundo wa Lebanon na eneo lote; na dhamana ya kufanikisha lengo hili “kubwa sana” ni nguvu mbili kubwa, yaani Saudi Arabia na Iran.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha