Alhamisi 28 Mei 2026 - 23:58
Wanafunzi wa Pakistan watoa heshima kwa wanafunzi walio uwawa kishahidi wa shule ya Minab Iran

Hawza/ Wanafunzi wa “Akademia ya Vikosi ya Rawalpindi” nchini Pakistan, walipohudhuria katika Nyumba ya Utamaduni ya Iran, walitoa heshima kwa wanafunzi mashahidi wa shule ya mji wa Minab pamoja na familia zao na taifa la Iran, na wakaonesha mshikamano wao.

Kwa mujibu wa ripoti ya Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, wanafunzi wa “Akademia ya Vikosi ya Rawalpindi” nchini Pakistan, walipohudhuria katika Nyumba ya Utamaduni ya Iran, walitoa heshima kwa wanafunzi mashahidi wa shule ya mji wa Minab nchini Iran pamoja na familia zao na taifa la Iran, na wakaonesha mshikamano wao.

Katika hafla hiyo, Hamza Mustafai, mmoja wa viongozi wa Jamaat Ahl al-Sunnah, Khalil kutoka Chama cha Jamaat-e-Islami, pamoja na shakhsia nyengine za kidini na kitamaduni za Pakistan walihudhuria.

Hamza Mustafai, seneta wa zamani na kiongozi mkuu wa Jamaat Ahl al-Sunnah alisema: Watoto wanapaswa kuwekwa mbali na vita na waelekezwe tu katika kutafuta elimu na kujenga mustakabali bora zaidi.

Alisisitiza kuwa; katika mafundisho ya Kiislamu, kulinda maisha si kwa watoto pekee, bali pia kwa wazee, wanyama, mimea, wanazuoni na watu wenye ulemavu kumetiliwa mkazo maalumu, na hata katika mazingira ya vita, kuheshimu haki zao ni jambo la lazima, lakini Marekani na Israel kwa kuvunja misingi yote ya kivita, waliwalenga watoto wasio na hatia wa shule ya Minab na kutekeleza uhalifu wa kivita.

Mustafai, huku akibainisha kwamba Iran ndiyo nchi pekee ambayo imetetea Uislamu katika medani zote na katika vita vya hivi karibuni, kwa kuishinda Marekani imeinua bendera ya Uislamu na kuwa shujaa wa Umma wa Kiislamu, aliongeza: Waislamu duniani wanaichukulia Iran kuwa shujaa wao na wanajivunia kusimama kwake imara na muqawama wake, na wanaiona nchi hiyo kuwa alama ya heshima, ushujaa na uthabiti mbele ya madola duniani.

Aliongeza: Watu wa Pakistan wanaelewa vizuri maumivu haya, kwa sababu huko Peshawar pia maadui wetu walishambulia shule moja na watoto wengi wakauwawa kishahidi, na kwa namna hiyo hiyo nchini Iran pia maadui wa Uislamu walishambulia shule ya Minab na kuwaua kishahidi watoto wasio na hatia.

Khalil, mwanachama wa Chama cha Jamaat-e-Islami Pakistan, katika hotuba yake alisema: Marekani na Israel ni nchi za kigaidi, na Waislamu wanapaswa kuhifadhi umoja na mshikamano wao na kujiepusha na maadui hawa wa Uislamu.

Aidha, alisisitiza kuwa; njia pekee ya kukabiliana na changamoto za ulimwengu wa Kiislamu ni kuimarisha umoja, mshikamano na maelewano kati ya nchi za Kiislamu, na kwamba aina yoyote ya mgawanyiko na hitilafu itawanufaisha maadui wa Uislamu.

Khalil aliongeza kuwa; mataifa ya Kiislamu yanapaswa kuchukua msimamo mmoja na madhubuti mbele ya dhulma na ukosefu wa haki duniani, na yasiruhusu haki za mataifa yaliyodhulumiwa kukanyagwa.

Shahid Jamil Qureshi, mkurugenzi wa “Akademia ya Vikosi ya Rawalpindi”, katika hafla hiyo alisema: Nafasi ya Nyumba ya Utamaduni ya Iran mjini Rawalpindi katika kuimarisha uhusiano wa Iran na Pakistan, kama nchi mbili ndugu na jirani, ni muhimu sana na yenye athari kubwa, na kuandaliwa kwa programu kama hizi kunaweza kuimarisha mahusiano ya kitamaduni na kupanua uhusiano wa kirafiki kati ya nchi hizi mbili.

Akiashiria kwamba Marekani na Israel kwa kuwaua kishahidi watoto wasio na hatia nchini Iran wamejiwekea doa kubwa la aibu katika historia ya dunia, na kwamba doa hilo litabaki milele, aliongeza: Katika hali hii, nafasi ya Iran ni ya kipekee sana, kwa sababu Iran ilisimama imara mbele ya madola ya dunia na ikayatupa matakwa yao yasiyo ya haki katika jaa la historia, na ikaithibitishia dunia kwamba mbele ya nguvu ya imani, hakuna nguvu yoyote inayoweza kusimama.

Mkurugenzi wa “Akademia ya Vikosi ya Rawalpindi” mwishoni mwa hotuba yake alisema: Shambulio dhidi ya shule ya Minab, baada ya Nagasaki na Hiroshima, ni moja ya uhalifu mkubwa zaidi wa kivita wa Marekani, na doa hili la aibu litabaki milele katika sura ya nchi hiyo.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha