Kwa mujibu wa Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, tovuti ya “Muungano wa Vijana wa Mapinduzi ya Februari 14” imetangaza kwamba vikosi vya utawala wa Aal Khalifa vimevamia kwa kiwango kikubwa nyumba za baadhi ya wanazuoni wa dini na shakhsia za kidini za jamii ya Kishia, na kutekeleza hatua ambayo wachambuzi wameitaja kuwa ni tukio hatari zaidi katika miaka ya hivi karibuni. Hatua hii inaonesha kiwango cha kuporomoka kwa hali ya haki za binadamu na kisiasa nchini Bahrain.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, waliokamatwa na wale ambao nyumba zao zimevamiwa hadi sasa ni hawa wafuatao:
Hujjatul Islam wal-Muslimin:
1. Sheikh Muhammad Sanqour
2. Sheikh Mahmoud Aalī
3. Sheikh Ali Saddadi
4. Sheikh Ali Hamidan
5. Sheikh Jassim Mu’min
6. Sheikh Ali Rahmah
7. Sheikh Hamed Ashour
8. Sheikh Fadhil Zaky
9. Sheikh Radhi Qaffas
10. Sheikh Munir Ma’touq
11. Sheikh Ghazi Sammak
12. Sheikh Sadiq Afiyah
13. Sheikh Ali Mutaghawi
14. Sheikh Muhammad Jawad Shahabi
15. Sheikh Hani Binnaa
16. Sheikh Jassim Khayyat
17. Sheikh Muhammad Kharsi
18. Sheikh Mahmoud Ashour
19. Sheikh Ayyoub Bahrani
20. Sheikh Isa Mu’min
21. Sheikh Jamil Aalī
22. Sayyid Muhammad Ghuraifi
23. Sheikh Ali Naji Hamli
24. Sheikh Baqir Hawaj
25. Sheikh Raed Satri
26. Sayyid Sadiq Maliki
27. Sheikh Hamzah Dairi
28. Sheikh Ali Hassan Suibai
29. Sheikh Hussein Mahrous
30. Sheikh Ali Salim
31. Sayyid Ahmad Ghuraifi
Kwa mujibu wa ripoti ya tovuti hiyo, operesheni hiyo haikuishia kwenye ukamataji pekee, bali pia mashambulizi ya kikatili yalifanyika ambayo yaliambatana na kuvunjiwa heshima watu hao. Katika mashambulizi haya yaliyoanza tangu alfajiri ya jana, familia na watoto wamepitia mazingira yaliyojaa hofu na taharuki. Mwenendo huu ni taswira ya sera ya kiusalama inayojengwa juu ya ukandamizaji na kuvunja irada ya jamii.
Katika sehemu nyingine ya ripoti hiyo imeelezwa kuwa; wanaharakati wanaamini kwamba yanayotokea yanazidi kuwa operesheni ya kawaida ya kiusalama ya muda mfupi, na kwa hakika yanafuatilia lengo la moja kwa moja dhidi ya utambulisho wa kidini na uwepo wa kijamii wa jamii ya Kishia nchini Bahrain. Hatua hizi zinafanyika katika mfumo wa sera endelevu ya kuiweka katika mashinikizo, kuitenga na kujaribu kuzinyamazisha sauti za kidini na kijamii zenye athari.
Kwa mujibu wa tovuti hiyo, hatua hizi zimezua wimbi la hasira na lawama kubwa, hasa kwa kuwa zimeandamana na uharibifu wa mali binafsi, mwenendo wa kudhalilisha familia pamoja na kuunda mazingira ya hofu katika maeneo yaliyolengwa.
Wachambuzi, wakinukuu tovuti hiyo hiyo, wanasisitiza kwamba; kuendelea kwa sera kama hii hakutakuwa na matokeo mengine isipokuwa kuongeza mgogoro wa ndani na kuongezeka mvutano wa wananchi, hususan katika hali ambayo ukosoaji dhidi ya mkabala wa “ngumi ya chuma ya kiusalama” na kulengwa kwa shakhsia za kidini na kijamii unaongezeka siku baada ya siku.
Tovuti ya “Muungano wa Vijana wa Mapinduzi ya Februari 14” mwishoni imeandika: Yanayotokea leo nchini Bahrain ni doa jipya la aibu katika faili la ukiukwaji wa haki za binadamu, na yanafichua ukubwa wa mkwamo ambao utawala wa Aal Khalifa umekumbana nao katika kukabiliana na jamii halisi ya Kishia; mkwamo ambao ni matokeo ya kutumia nyenzo za ukandamizaji na ufuatiliaji badala ya kuheshimu haki na uhuru wa msingi.
Inafaa kutajwa kuwa; utawala wa Aal Khalifa nchini Bahrain tangu kuanza kwa Vita vya Ramadhani dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, umeongeza mashambulizi ya ukandamizaji na ukamataji mkubwa dhidi ya wapinzani, wanaharakati na wanazuoni wa dini.
Maoni yako