Jumamosi 9 Mei 2026 - 16:40
Utamaduni wa jihadi ni utamaduni wa ushindi na wa ukombozi

Hawza/ Khatibu wa Swala ya Ijumaa ya Tehran amesema kwamba; utamaduni wa Mtume (saww) ndio huo huo utamaduni wa jihadi ambao Mapinduzi ya Kiislamu yamesimama nao na yataendelea kusimama nao, na akasema: “Jihadi maana yake ni ushindi, na Mwenyezi Mungu ndiye mnunuzi wa mujāhidina wa njia ya haki.”

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza kutoka Tehran, Seyyed Ahmad Khatami katika khutba za ibada na siasa za Swala ya Ijumaa mjini Tehran, sambamba na kufafanua vipengele mbalimbali vya utamaduni wa Mtume Mtukufu (saww), aliuelezea kuwa ni sababu ya kuokoa na msingi wa kudumu kwa Mapinduzi ya Kiislamu, na akasema: “Utamaduni huu ndio huo huo utamaduni wa jihadi ambao lau usingekuwepo, Mapinduzi ya Kiislamu nayo yasingeweza kubaki na kuendelea.”

Akifafanua maana ya jihadi, aliielezea kuwa ni sawa na ushindi wala si kushindwa, na akaongeza: “Katika medani ya jihadi, mnunuzi mkuu ni Mwenyezi Mungu; tofauti na shetani ambaye humsukuma mwanadamu kuelekea maangamizi, Mwenyezi Mungu ndiye mnunuzi wa mujāhidina wanaopiga hatua katika njia Yake.”

Khatibu wa Swala ya Ijumaa ya Tehran, aliwaita wapiganaji waliopo katika medani za mapambano kuwa ni vipenzi vya Mwenyezi Mungu, na akasisitiza: “Wale ambao wanasimama kwa roho ya jihadi kando ya vizindua makombora, wako chini ya hifadhi ya mapenzi na uangalizi wa Mwenyezi Mungu, na wanasimama imara mbele ya maadui kama ukuta wa chuma.”

Seyyed Ahmad Khatami huku akisisitiza ushindi wa daima wa mujāhidina alisema: “Wale watu wanaofanya biashara na Mwenyezi Mungu hupata ustahiki wa kuwepo katika medani za mapambano na kutoa roho zao katika njia ya Mwenyezi Mungu, na watajumuishwa katika malipo na thawabu kubwa kutoka kwa Mola.”

Aliuita utamaduni wa jihadi kuwa kwa hakika ni utamaduni wa maisha na uhai, na akasisitiza umuhimu wake mkubwa katika kuendelea njia ya saada.

Utamaduni wa jihadi ndio msingi wa uwepo wa wananchi kwa siku 70 uwanjani

Seyyed Ahmad Khatami huku akirejea uwepo wa wananchi kwa takribani siku 70 uwanjani, alieleza kuwa; uimara huu umetokana na utamaduni wa jihadi liyofunzwa kutoka kwa Mtume Mtukufu wa Uislamu (saww).

Aliuelezea utamaduni huu kuwa ndio sababu kuu ya uwepo wa wananchi katika njia ya Mapinduzi na maadili yake.

Khatibu wa Swala ya Ijumaa ya Tehran, katika sehemu nyingine ya hotuba zake aliwashukuru kwa dhati wasanii wa kidini wa nchi ya Iran, kwa kutumia sanaa yao katika kueneza maadili ya juu ya Mapinduzi ya Kiislamu.

Pia aliishukuru Idhaa na Televisheni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa shughuli zake kubwa na uwepo wake wenye athari katika matukio mbalimbali, hususan katika siku nyeti za vita. Aidha, Seyyed Ahmad Khatami alimshukuru msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje kwa majibu yake madhubuti na yenye kustahiki pongezi.

Katika mwendelezo wa hotuba yake, Seyyed Ahmad Khatami aliishukuru Jumuiya ya Mwezi mwekundu na jumuiya ya madaktari wa Irwn, kwa huduma zao zenye thamani. Pia akirejea hali ngumu ya mhimili wa Muqawama, alizishukuru nguvu hizi kwa juhudi zao ambazo zimesababisha mchana ugeuke usiku kwa utawala vamizi wa Israel.

Seyyed Ahmad Khatami alisema kwamba: Kuuelekea na kuupenda kwa kiwango kikubwa mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu kutoka kwa wananchi ni miongoni mwa vielelezo vya fadhila na uangalizi wa Mwenyezi Mungu Mtukufu.

“Mazungumzo yenye heshima” ndiyo matakwa makuu ya wananchi katika medani

Seyyed Ahmad Khatami katika khutba za Swala ya Ijumaa ya Tehran, huku akirejea ujumbe uliobadilishana kupitia Pakistan kuhusu mazungumzo, alizielezea juhudi zilizofanywa katika suala hili kuwa ni za kustahiki kuthaminiwa, na akasema: “Matakwa makuu ya wananchi ambao kwa takribani siku 70 wamekuwa barabaranj ni kufikiwa kwa mazungumzo yenye heshima.”

Aliuambia ujumbe wa mazungumzo wa nchi yao kuwa: “Katika mchakato wa mazungumzo haya, msilegeze hata chembe moja kutoka katika misingi na misimamo yenu ya asili.”

Seyyed Ahmad Khatami kuhusu “kipindi cha ukimya” kilichotajwa na Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi alisema: “Kipindi hiki si usitishaji vita, bali ni kipindi cha ukimya. Maadamu maadui kama Donald Trump wapo, ni lazima kusimama imara mbele yao na hatupaswi kudhani kwamba simulizi limekwisha. Aidha tunawaomba wapiganaji kwamba mikono yao ibaki daima juu ya vichocheo vya silaha.”

Khatibu wa Swala ya Ijumaa ya Tehran huku akirejea vita vya kisaikolojia vinavyoongozwa na maadui alisema: “Vita vya kisaikolojia ni sehemu muhimu ya mapambano, na maadui wanavitumia kudhoofisha morali na kueneza kukata tamaa. Wananchi wanapaswa kuwa macho, kwa sababu maadui wanataka kuwaonesha nyinyi kuwa mmechoka na kueneza habari za uongo pamoja na uchambuzi potofu; hivyo wasiyasikilize maneno yao.”

Alisema: “Maadui wanataka kuleta hitilafu na mgawanyiko kati ya safu za taifa, lakini tunamshukuru Mwenyezi Mungu, kuna umoja kamili kati ya wananchi na viongozi wa nchi.”

Seyyed Ahmad Khatami aliendelea kusema kwamba; Donald Trump anayejulikana kama “mla watoto”, anaendelea kuitishia Iran kila mara, lakini akasema kwamba vitisho hivyo havina matokeo yoyote.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha