Jumapili 26 Aprili 2026 - 22:30
Msimamo thabiti wa Sheikh Maher Hammoud katika kuunga mkono mhimili wa muqawama

Hawza/ Rais wa Umoja wa Kimataifa wa Wanazuoni wa Muqawama nchini Lebanon amesema: Sisi tuko pamoja na Iran na mhimili wa muqawama, kwa sababu wao wamesimama katika upande wa haki pamoja na Palestina na dhidi ya Marekani na jinai zake.

Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Sheikh Maher Hammoud, Rais wa Umoja wa Kimataifa wa Wanazuoni wa Muqawama nchini Lebanon, katika msimamo wake wa kisiasa wa kila wiki alisema: Sisi tuko pamoja na Iran na muqawama si kwa sababu viongozi wao ni wenye sura nzuri, wenye mvuto wa kisiasa au matajiri, bali kwa sababu wamesimama katika upande wa haki pamoja na Palestina na dhidi ya Marekani na jinai zake, na wako pamoja na mataifa yaliyodhulumiwa.

Sheikh Hammoud alisisitiza kuwa: Uboreshaji huu una sababu kadhaa, miongoni mwazo ni ushindi au uthabiti wa Iran katika makabiliano, na kushindwa kwa madai ya Trump kuhusu kuangamizwa kwa mpango wa nyuklia wa Iran, pamoja na msimamo wa Saudi Arabia ambao unapinga kutoa misamaha ya bure, na kwa njia isiyo ya moja kwa moja umeashiria mabadiliko ya serikali ya Lebanon.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha