Jumamosi 18 Aprili 2026 - 19:30
Trump baada ya kushindwa vitani sasa anakabiliwa na kushindwa ndani ya nchi; hatimaye Iran imeshinda

Hawza/ Hujjatul-Islam wal-Muslimin Sayyid Sadr al-Din Qabanchi alisema: Trump baada ya kushindwa vitani sasa anakabiliwa pia na kushindwa ndani ya nchi, na hatimaye Iran imeshinda na madola ya kibabe yamelazimika kuomba kusimamishwa kwa vita.

Kwa mujibu wa Idara ya tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, Hujjatul-Islam wal-Muslimin Sayyid Sadr al-Din Qabanchi, Imamu wa Ijumaa wa Najaf Ashraf, katika khutba za Swala ya Ijumaa alizozitoa katika Husseinia Kuu ya Fatimiya mjini Najaf Ashraf, alisema: Tunakumbushia jinai ya Anfal ambayo ndani yake kati ya watu (50,000) hadi (100,000) wa ndugu zetu Wakurdi, wanaume na wanawake, waliuawa, na ndani yake vijiji (4000) viliharibiwa; tukio hili lilitokea mwaka 1988 Miladia (1366 Hijria Shamsia), na lilikuwa ni uhalifu wa aina ya mauaji ya kimbari ya kibinadamu uliotekelezwa na utawala wa Baath.

Katika masuala ya kimataifa, alisema: Papa Leo wa kumi na nne amelaani vita dhidi ya Iran, na pia ameilaani sera ya kutumia dini katika masuala ya kisiasa na kiuchumi. Kwa mara ya kwanza tunashuhudia mvutano kati ya mamlaka ya kidini na uongozi wa kisiasa katika jamii ya Magharibi. Kauli yetu ni kwamba tunamshukuru Papa Leo wa kumi na nne.

Imamu wa Ijumaa wa Najaf Ashraf alisisitiza: Trump baada ya kushindwa vitani sasa anakabiliwa pia na kushindwa ndani ya nchi, na hatimaye Iran imeshinda na madola ya kibabe yamelazimika kuomba kusimamishwa kwa vita. Trump anazihimiza nchi tano za mwambao wa Ghuba ya Uajemi (Saudi Arabia, Imarati, Kuwait, Bahrain, Qatar) zilipie fidia kwa Iran, ilhali Iran tayari imefikia ushindi wake na kulazimisha masharti yake.

Ushindi wa Hizbullah, kusimama kwa vita na kushindwa kwa Israel

Hujjatul-Islam wal-Muslimin Sayyid Sadr al-Din Qabanchi katika sehemu nyingine ya khutba yake alirejea ushindi wa Hizbullah nchini Lebanon, kusimama kwa vita na kushindwa kwa Israel, na akasema: Tunawashukuru vijana wetu wa Hizbullah. Watu wa Lebanon, hasa Mashia, walivumilia vita ngumu ambapo familia (1,200,000) zililazimika kuhama, lakini hatimaye irada ya imani iliyo thabiti ya Hizbullah nchini Lebanon ilishinda.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha