Jumanne 14 Aprili 2026 - 20:02
Kiongozi mtukufu wa Kanisa Katoliki duniani; sisi wana hawza tunathamini misimamo hii ya kimaadili na kibinadamu mliyoionesha, na tunaamini hivyo, umeendelea kubaki mwaminifu kwa ujumbe wa kweli wa Ukristo

Hawza/ Katika zama ambazo ukimya mbele ya dhulma umegeuka kuwa lugha ya kawaida ya wenye nguvu na wale wanaodai haki za binadamu, na viongozi wengi duniani wamenyamaza au katika mizunguko ya mahesabu ya kisiasa ndimi zao zimekwama na kupata kigugumizi cha maslahi, sauti yako ya wazi na ya ujasiri katika kulaani mabomu dhidi ya wasio na hatia na katika kunyang’anya uhalali wa mauaji ya watu wasio na ulinzi, na katika kuunga mkono haki na uhuru, imeng’aa kama nuru katika giza hili nene la usiku. Sisi wana Hawza, tunathamini misimamo yako hii ya kimaadili na kibinadamu na tunaamini hivyo.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, maandishi ya ujumbe wa pongezi na shukrani ya Ayatollah Arafi, Mkurugenzi wa Hawza Iran, aliyomwandikia Papa Leone wa kumi na nne ni kama ifuatavyo:

“Na utawakuta walio karibu mno kwa mapenzi ni wale wanao sema: Sisi ni Manasara. Hayo ni kwa sababu wapo miongoni mwao makasisi na wamonaki, na kwa sababu wao hawafanyi kiburi.”

Mheshimiwa Papa Leone wa Kumi na Nne: Kiongozi mtukufu wa Kanisa Katoliki duniani,

Kwa salamu na heshima,

Katika zama ambazo ukimya mbele ya dhulma umegeuka kuwa lugha ya kawaida ya wenye nguvu na wanaodai haki za binadamu, na viongozi wengi duniani wamenyamaza au katika mizunguko ya mahesabu ya kisiasa ndimi zao zimekwama katika kigugumizi cha maslahi, sauti yako ya wazi na ya ujasiri katika kulaani mabomu dhidi ya wasio na hatia na kunyang’anya uhalali wa mauaji ya watu wasio na ulinzi, pamoja na kuunga mkono haki na uhuru, imeng’aa kama nuru katika giza hili nene la usiku.

Sisi ndani ya Hawza, tunathamini misimamo yako hii ya kimaadili na kibinadamu na tunaamini kwamba:

Kwanza: Umeendelea kuwa mwaminifu kwa ujumbe wa kweli wa Ukristo kwa sababu Nabii Isa Masihi (amani ya Mungu iwe juu yake), ambaye sisi Waislamu tunamhesabu kuwa ni miongoni mwa Mitume wakuu wa Mungu na tunamwamini na kumpenda, alikuwa mjumbe wa amani, rehema na mtetezi wa wanyonge. Kile unachokitamka leo ni undani wa ujumbe ule ule alioubeba Masihi (a.s.). Leo umeonesha kwamba; kiti cha Vatikani kinaweza kuwa mahali pa kupaza sauti ya haki, si madhabahu ya kunyamazia dhulma; na matarajio madhubuti ya taasisi za kielimu, kidini, vyuo vikuu na wanaomuamini Mungu pamoja na wanyonge duniani kutoka kwako ni kuendeleza na kufuatilia misimamo hii na kuwatetea wanyonge duniani.

Pili: Umethibitisha kuwa dhamiri ya kidini bado ipo hai.

Katika zama ambazo watu wengi wanajaribu kuisukuma dini pembeni mwa uwanja wa maisha ya maadili ya mwanadamu na kuifanya kuwa jambo la kibinafsi lisilo na athari, msimamo wako wa kutetea maisha ya wanadamu wasio na hatia ni ushahidi hai kwamba, dhamiri ya kidini bado inaweza kuwa sauti yenye nguvu zaidi ya maadili duniani. Kuwatisha madhalimu kwa kuwaonya na adhabu ya Mungu kupitia ulimi wako kunakumbusha ile desturi ya pamoja ya Manabii ambao hawakunyamaza mbele ya wanyanyasaji.

Tatu: Tunakuunga mkono kwa ajili ya kuzizungumzia dini, kwa ajili ya kutetea ubinadamu na maadili ya kimungu.

Qur’ani Tukufu inatuita kwenye neno la pamoja miongoni mwa dini: “Sema: Enyi Watu wa Kitabu! Njooni kwenye neno lililo sawa baina yetu na baina yenu.” Leo hii neno hilo la pamoja ni kutetea heshima ya maisha ya mwanadamu na kusimama dhidi ya jinai na dhulma. Sisi wana Hawza tunatangaza kuwa, tuko tayari kwa ushirikiano wa kina zaidi na Vatikani ili kuibadilisha sauti hii ya pamoja ya kimaadili kuwa harakati pana ya kuwatetea wanyonge duniani, na tunakumbushia mazungumzo yaliyopita kati ya Hawza ya Qom na Vatikani na kuonesha utayari wa kuyaendeleza.

Tunaamini kwamba, Manabii wa Mungu kuanzia Ibrahim, Musa, Isa hadi Muhammad (rehma za Mungu ziwe juu yao wote) wote wamekunywa kutoka chemchemi moja ya nuru na utume wao ulikuwa wa kulinda hadhi ya mwanadamu, kupambana na dhulma na kuwaongoza wanadamu. Kile ambacho wewe na sisi tunakifanya leo ni kutekeleza amana hii ya pamoja na kitarekodiwa katika historia.

Kwa heshima na shukrani nyingi,

Alireza Arafi
Mkurugenzi wa Hawza Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha