Kwa mujibu wa idara ya kimataifa ya Shirika la Habari la Hawza, hafla ya kumbukumbu ya mashahidi wa Iran ilifanyika katika eneo la Halkalı, Istanbul.
Katika hafla hiyo walihudhuria: Hujjat al-Islam wal-Muslimin Sheikh Salahuddin Ozgunduz; Hujjat al-Islam wal-Muslimin Dkt. Akbar Fallah-Nejad, mwakilishi wa kitengo cha kimataifa cha ofisi kuu ya kiongozi mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran; Ahmad Muhammadi, balozi mdogo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran huko Istanbul; pamoja na shakhsia mbalimbali, wawakilishi wa vyama vya kisiasa, wakuu na wakurugenzi wa asasi za kiraia, na maelfu ya wapenzi wa Ahlul-Bayt (as) na mhimili wa muqawama.
Alhamisi tarehe 9 Aprili (20 Farvardin), baada ya swala ya Alasiri, maelfu ya wafuasi wa Ahlul-Bayt (as) walikusanyika katika ua wa Kituo cha Utamaduni cha Msikiti wa Zaynabiyya na kisha wakaelekea kwenye Kituo cha Utamaduni cha Yahya Kemal Beyatli, huku njiani wakifanya maombolezo na kupaza kauli mbiu “Labbayka ya Hussein”.
Hafla hiyo ilianza kwa dakika moja ya kimya kwa kumbukumbu ya mashahidi wote, kisha ikaendelea kwa tilawa ya Qur’ani Tukufu.
Baadaye, Ahad Talan, rais wa Muungano wa Wanazuoni wa Ja‘fari, katika hotuba yake ya kuwakaribisha alisema: “Vita ambavyo Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ilipigana dhidi ya mabeberu wakatili na Wazayuni wa kumwaga damu havikuwa tu vita vya kulinda nchi na taifa; bali vilikuwa pia mapambano ya kutetea dini na ubinadamu. Kwa hiyo, mapambano haya ya heshima yameandikwa katika historia na yatabaki kuwa mfano kwa vizazi vijavyo.”
Aliongeza: Kama ilivyo katika kila vita, vita hivi visivyo vya haki pia vimesababisha hasara kubwa za mali; lakini kwa msaada wa mataifa rafiki na ndugu, na kwa juhudi za watu wa Iran, nchi hii itajengwa upya hivi karibuni. Talan pia alitoa shukrani kwa misimamo na uungaji mkono wa watu na viongozi wa Jamhuri ya Uturuki dhidi ya wavamizi.
Kisha, Hasan Babur, rais wa Ja‘fari-Der (CAFERİDER), alisema: “Muundo wa kibeberu na Kizayuni kwa kumwaga tani kadhaa za mabomu, uliwaua kishahidi kiongozi mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran pamoja na wenzake na makamanda wake, na wakati huo huo takriban wasichana 180 wenye umri kati ya miaka 7 hadi 12 walipoteza maisha katika shambulizi dhidi ya shule ya msingi.”
Aliongeza kuwa: Katika kipindi hiki cha siku arubaini, maelfu ya watu nchini Iran na Lebanon wamepata shahada, nasi tunaheshimu kumbukumbu ya wote hao na kuwaombea rehema.
Hujjat al-Islam wal-Muslimin Dkt. Fallah-Nejad pia katika hotuba yake alisema: “Watu wa Iran katika siku arubaini zilizopita wamekuwa katika huzuni kubwa, na usiku wamekuwa wakipaza sauti katika viwanja wakitaka kulipiza kisasi kwa mashahidi wao. Pamoja na hayo, hawajawahi kunyenyekea mbele ya ubeberu na Uzayuni, na jeshi la nchi limesimama imara kikamilifu dhidi ya mkondo huu.”
Alisisitiza: Katika siku hizi ngumu, mataifa mbalimbali, Waislamu na wapenda uhuru duniani wamesimama pamoja na watu wa Iran, na hasa Jamhuri ya Uturuki kwa makundi yake yote—Wasunni, Mashia na Alavi—wsmeonesha mshikamano wao.
Katika mwendelezo wa hafla hiyo, Hujjat al-Islam wal-Muslimin Sheikh Salahuddin Ozgunduz alisema: “Katika siku ya kwanza ya vita hivi vya siku arubaini, Sayyid mmoja kutoka kizazi cha Bibi Fatima (as), Imamu Ali (as) na Imamu Hussein (as), pamoja na takriban wasichana wadogo 180 waliuawa kishahidi huko Minab, lakini leo ubeberu na Uzayuni wameshindwa mbele ya damu yao.”
Aliongeza kuws: “Vita hivi vingaliweza kugeuzwa kuwa mgogoro kati ya Shia na Sunni au Waarabu na Waajemi, lakini lengo hili halikutimia, na Jamhuri ya Uturuki haikuruhusu mwelekeo huo potofu.”
Ozgunduz pia, akirejea maendeleo ya kikanda na kimataifa, alisisitiza umuhimu wa kuwa macho dhidi ya njama za kugawanya, na kusema: “Mataifa hayapaswi kuangukia katika mitego ya miradi ya kugawanywa ya ubeberu na Uzayuni.”
Maoni yako