Jumapili 12 Aprili 2026 - 18:30
Muqawama utaendelea hadi pumzi ya mwisho; tunawaomba viongozi waache kutoa upendeleo wa bure

Hawza/ Sheikh Naim Qasim, Katibu Mkuu wa Hizbullah, alituma ujumbe kwa Walebanon thabiti na wanaojitolea, na akasema: Ninatoa pole kwa familia zetu zenye subira na uthabiti kote Lebanon kwa kupaa kwa mashahidi watukufu miongoni mwa wanaume, wanawake, watoto na mujahidina.

Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Sheikh Naim Qasim, Katibu Mkuu wa Hizbullah, alituma ujumbe kwa Walebanon thabiti na wanaojitolea, na akasema: Ninatoa pole kwa familia zetu zenye subira na uthabiti kote Lebanon kwa kupaa kwa mashahidi watukufu miongoni mwa wanaume, wanawake, watoto na mujahidina, na ninamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu awape daraja za juu kabisa za rehema; kwa kuwa damu safi waliyoitoa tunaiona kuwa ni sababu ya kusaidia kupata heshima na ushindi dhidi ya adui Muisraeli–Mmarekani dhalimu na mwenye kiburi. Vilevile ninamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu awaponye majeruhi uponyaji wa haraka, na azipe familia subira, azma na tawfiq.

Aliongeza kuwa: Adui Muisraeli alishindwa kukabiliana ana kwa ana katika uwanja wa mapambano na mashujaa jasiri wa muqawama, na hakuweza kutekeleza operesheni ya ardhini kama alivyokuwa akitangaza mara kwa mara. Askari na maafisa wake waliangamizwa katika mitego ya mujahidina, na magari yake yakaharibiwa katika milango ya miji na vijiji.

Sheikh Qasim aliendelea: Adui alibadilisha malengo yake mara kadhaa; wakati mwingine kufika Litani, wakati mwingine kusonga mbele kwa kiwango kidogo, mara nyingine kudhibiti kwa moto, na mara nyingine kutegemea moto na uharibifu. Katika uvamizi wake wa siku arubaini, hakufanikiwa kuzuia kurushwa kwa makombora, mizinga na ndege zisizo na rubani kuelekea makazi ya walowezi wa karibu na wa mbali hadi Haifa na zaidi ya hapo.

Katibu Mkuu wa Hizbullah alisisitiza: Adui alishangazwa na mbinu za muqawama, unyumbufu wa harakati za mujahidina, uwezo wao wa kujihami na ujasiri wao wa kishujaa wa kipekee. Ilidhihirika kwamba kukusanya askari laki moja wa Kizayuni hakutasaidia utekaji, bali watageuka kuwa miili na vipande vilivyokatika; na wale waliobaki uwanjani wanaishi kwa hofu na wasiwasi, hawajui ni lini watakufa? Ni lini watatekwa? Au ni lini amri ya kurudi nyuma itatolewa? Kwa sababu hawana uwezo wa kudumu katika ardhi takatifu ya kusini yenye ukarimu na inayolea mashahidi.

Alisema kwamba: Kwa muda wa siku arubaini, adui anaendelea kuongeza kushindwa kwake; makazi yake yamejaa maumivu na hofu; mipango yake imevurugika na viongozi wake kila siku wanatoa vitisho kwa sauti kubwa lakini athari ndogo.

Sheikh Qasim alisisitiza: Adui siku ya Jumatano huko Beirut, Dhahieh, Kusini, Biqaa na Mlima Lebanon, na kila mahali, aligeukia jinai ya umwagaji damu kwa kulenga raia katika maeneo yenye msongamano wa watu, miji na vijiji, ili kuficha udhaifu wake uwanjani. Lakini watu wa Lebanon ni wenye nguvu zaidi na thabiti kuliko anavyodhani adui; waliokimbia makazi yao walionesha mfano wa fahari na ari ya juu; waliowapokea walionesha sura tukufu zaidi za ubinadamu na uraia; na mujahidina katika medani za mapambano ni ngome imara inayovunja ndoto na matarajio ya Wazayuni.

Alisema: Muqawama utaendelea hadi pumzi ya mwisho, na kukimbilia vijana uwanjani na kutouacha ni dirisha la matumaini na heshima. Wahanga hawa wanatufanya tushikamane zaidi na ukombozi wa nchi yetu na heshima yetu. Hatutarejea kamwe katika hali ya awali, na tunawaomba viongozi waache kutoa upendeleo ya bure.

Sheikh Qasim alisisitiza pia: Sisi kwa pamoja—serikali, jeshi, wananchi na muqawama—tutailinda nchi yetu, tutarejesha mamlaka yake na tutamfukuza mvamizi. Vitisho na silaha zao havitutishi; kwa sababu sisi ni wamiliki wa ardhi hii na tuna imani, azma na uwezo wa kuzuia utekelezaji wa malengo yao. Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema:
(کَتَبَ اللَّهُ لَأَغْلِبَنَّ أَنَا وَرُسُلِی  إِنَّ اللَّهَ قَوِیٌّ عَزِیزٌ)
“Mwenyezi Mungu ameandika kwamba bila shaka Mimi na Mitume wangu tutashinda; hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mwenye kushinda.”

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha