Kwa mujibu wa kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Abu Alaa al-Wala’i, Katibu Mkuu wa Vikosi vya “Sayyid al-Shuhada” vya Iraq, siku ya Jumatano aliutaka uongozi wa “Mhili wa Muqawama wa Kiislamu” kuilenga Israel katika kujibu mashambulizi ya mabomu dhidi ya Lebanon na ukiukaji wa usitishaji vita uliotangazwa jioni ya jana kati ya Iran na Marekani.
Al-Wala’i katika taarifa yske alisema: “Netanyahu aliyeshindwa, kwa ajili ya kuficha kushindwa kwake kihistoria mbele ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na mhimili wa muqawama katika vita ya nne ya ‘Ahadi ya Kweli’, amefanya mauaji dhidi ya watu wetu wa Lebanon wasio na ulinzi.”
Aliongeza kuwa: “Ndugu wapiganaji katika chumba cha operesheni cha uongozi wa mhimili na umoja wa medani wanapaswa kujibu kwa utawala huu haram ambao umevunja usitishaji vita na kuwaua watu wetu wasio na hatia na wasio na ulinzi nchini Lebanon. Utawala huu haram lazima ulipe gharama yake kwa jibu la pamoja na la kutetemesha kutoka kwa vikosi vyote vya muqawama.”
Katibu Mkuu wa vikosi hivyo alisisitiza: “Mhili wa muqawama una zana muhimu za kujibu mashambulizi haya ya kinyama ya Kizayuni dhidi ya Wale banoni, tutavunja kiburi chao cha uongo.”
Al-Wala’i alisisitiza ulazima wa kuendelea kufungua uwanja wa mapambano dhidi ya utawala haram ambao hauheshimu sheria za kimataifa, na pia dhidi ya nchi zinazofanya mapatano ambazo ndani yake kuna maslahi ya utawala wa Kizayuni, kama vile Falme za Kiarabu (UAE), Bahrain na nchi nyingine za eneo hilo.
Maoni yako