Jumatatu 6 Aprili 2026 - 16:40
Mikoa 12 ya Iraq yashuhudia maandamano dhidi ya uchokozi wa Marekani na Israel dhidi ya Iran

Hawza/ Maandamano ya Harakati ya Sadri yamefanyika kupinga “uchokozi wa Marekani na Israel” dhidi ya baadhi ya nchi za Kiislamu.

Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, maandamano ya Harakati ya Sadri yamefanyika katika mikoa 12 ya Iraq kupinga “uchokozi wa Marekani na Israel” dhidi ya baadhi ya nchi za Kiislamu.

Waandamanaji walikusanyika katika maeneo yaliyokuwa yameainishwa mapema; miongoni mwake ni Baghdad (Uwanja wa Tahrir), Basra (Daraja la al-Tarbiya), Maysan (Barabara ya Dijla), Dhi Qar (Uwanja wa al-Haboubi), Wasit (Uwanja wa Baraza), Muthanna (Uwanja wa Sherehe), Diwaniyah (Mzunguko wa Saa), Babil (Barabara ya Arbaeen), Karbala (Mzunguko wa al-Tarbiya), Diyala (Uwanja wa al-Fallaha), Kirkuk (Mzunguko wa Serikali ya Kale), na Nineveh (Bartella–Erbil).

Halem al-Fatlawi, mwakilishi wa Harakati ya Sadri katika maandamano ya Kirkuk, alisema: Wito uliotolewa na kiongozi wa harakati hiyo, Muqtada al-Sadr, unayahusisha makundi yote ya wananchi wa Iraq katika mikoa yote ili washiriki katika maandamano ya amani yanayolaani mashambulizi dhidi ya Palestina, Lebanon, Iran na Yemen, pamoja na Iraq.

Kwa upande wake, Ali Jaafar, mmoja wa washiriki wa maandamano hayo, alisema: Maandamano haya ni ujumbe wazi kwa dunia kwamba; watu wa Iraq wanakataa aina zote za uchokozi dhidi ya nchi na mataifa. Aliongeza kuwa; ushiriki mkubwa kutoka makundi yote ya Kirkuk unaonesha umoja wa safu ya Iraq.

Kiongozi wa harakati ya kitaifa ya Kishia, Sayyid Muqtada al-Sadr, Jumatatu iliyopita aliwataka raia wa Iraq kushiriki katika maandamano ya kulaani “uchokozi wa Marekani na Israel” siku ya Jumamosi katika mikoa yote—isipokuwa Najaf.

Mikoa 12 ya Iraq yashuhudia maandamano dhidi ya uchokozi wa Marekani na Israel dhidi ya Iran

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha