Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza kutoka Tehran, Mtukufu Ayatullah Sayyid Mujtaba Khamenei, Kiongozi wa Mapinduzi Iran, katika ujumbe wake ametoa shukrani zake za dhati kwa Mar'aji' wa juu wa kidini na wananchi wa Iraq kutokana na msimamo wao wa wazi dhidi ya uvamizi dhidi ya Iran na kuiunga mkono nchi hiyo.
Katika siku za hivi karibuni, Marji' wa taqlid Ayatullah al-Udhma Sayyid Ali Sistani, kupitia tamko alilolitoa, ametoa wito kwa Waislamu kuwasaidia wananchi wa Iran na Lebanon.
Inatajwa kuwa ujumbe wa Ayatullah Sayyid Mujtaba Khamenei, Kiongozi Mtukufu wa Mapinduzi, uliwasilishwa kwa Sheikh Humam Hammoudi, Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Kiislamu la Iraq, na Muhammad Kazem Al‑Sadiq, Balozi wa Iran mjini Baghdad, wakati wa mkutano wao.
Maoni yako