Kwa mujibu wa kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Hujjatul-Islam wal-Muslimin Sayyid Sadruddin Qabanchi, Imamu wa Ijumaa wa Najaf Ashraf, katika hotuba ya Swala ya Ijumaa iliyotolewa katika Husayniyya al-A’dham Fatimiyya Najaf Ashraf, huku akisisitiza kuwa; kupanga safu katika mapambano haya kunapaswa kuwa upande wa haki, alisema: Kufungwa kwa chuo cha dini (hawza) ilikuwa hatua ya kuonesha mshikamano na kusimama upande wa haki na kuepuka kuchukua msimamo wa watazamaji. Vilevile, msaada wa maeneo matukufu (Atabat Muqaddasa) na tamko la Marji' mkubwa wa Iraq, Ayatullah Sistani, kuhusu wajibu wa kifaya wa kuwasaidia waathiriwa wa vita vilitolewa; na kama ilivyo katika tamko lake, kulikuwa na kukemea uvamizi dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, na tunapaswa pia kuwashukuru wananchi wa Iraq.
Akiashiria kuwa mapambano yako kwenye hatua ya mabadiliko makubwa, aliongeza: Adui ametishia kwamba wanajeshi wa majini (Marines) wataingia katika ardhi ya Iran, ilhali Iran imeandaa wapiganaji milioni moja kukabiliana nao. Masharti ya Iran yalikuwa masharti ya Kiislamu: la kwanza, kurejeshwa Palestina kwa watu wake; la pili, kufidiwa hasara za vita vya uvamizi; na la tatu, kufikishwa mahakamani viongozi wa utawala wa Kizayuni.
Kutoridhika watu wa Iraq kutokana na kucheleweshwa kwa uchaguzi wa rais na waziri mkuu
Imamu wa Ijumaa wa Najaf Ashraf alisema: Wananchi wa Iraq hawaridhishwi na uteuzi wa rais na waziri mkuu kucheleweshwa na makundi mengi ya kisiasa ya Kishia na Kisunni; kucheleweshwa huku kumeiweka serikali katika hali ya matatizo ya kisheria. Vilevile, wananchi wa Iraq hawajafurahishwa na msimamo wa serikali kuhusu mapambano yanayoendelea Iran na Lebanon. Watu wa Iraq wanatarajia uungaji mkono wa kidiplomasia, kifedha, na kimtandao wa habari kwa Iran na Lebanon.
Alisema: Marji' mkubwa wa Iraq ametangaza msimamo wake, watu wa taifa pia wamesema neno lao, na Hashd al-Shaabi nao wametoa msimamo wao; sasa ni zamu ya serikali ya Iraq kuchukua msimamo wa kimatendo.
Hujjatul-Islam wal-Muslimin Sayyid Sadruddin Qabanchi, aliitaka serikali ya Iraq kusitisha utoaji wa mafuta bure kwa Jordan; mafuta ambayo Jordan huwapatia utawala wa Kizayuni.
Maoni yako