Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Sheikh Mustafa Mals, Rais wa Umoja wa Mshikamano wa Kitaifa wa Lebanon, katika kongamano la pili la kimataifa "Shahidi Sayyid Ali Husseini Khamenei; Imam wa Umoja, mlinganiaji wa Quds na Shahidi wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani," lililoandaliwa siku ya (Jumatano) na Jumuiya ya kukurubisha umoja wa dini za Kiislamu, alizungumzia kuhusu Siku ya Quds na suala la Palestina na kusema: "Umoja wa Umma wa Kiislamu ni wajibu wa Qur'ani na ombi la Sheria, na una manufaa kwa umma wa Kiislamu, na ndio sababu unayopaswa kuwa kipaumbele kikubwa ili umma wa Kiislamu uwe umma mmoja."
Alisisitiza kuwa: "Tunaishi katika zama ambazoo maadui wamejumuisha nguvu zao zote ili kuwapokonya Waislamu haki zao na ardhi yao. Hii ni kutokana na mgawanyiko ambao umma wa Kiislamu umeingia, jambo ambalo limemwezesha adui kuwa na ujasiri wa kuwashambulia na kuwadhalilisha Waislamu. Hivyo, lazima tutoke kwenye mgawanyiko huu na tuungane."
Rais wa Umoja wa Mshikamano wa Kitaifa wa Lebanon aliongeza kusema: "Kila taifa linaloungana linayalazimisha mataifa mengine duniani kuliheshimu, kinyume chake, taifa lolote linalokumbwa na mgawanyiko na kutengana linawafanya watu wengine kuwa na ujasiri wa kuwadhihaki, na linakuwa tenge rahisi kwa ajili ya kumezwa."
Alisema kuwa: "Suala la Palestina ni suala ambalo linaonesha kila aina ya dhuluma, unyanyasaji, na uasi. Ni suala ambalo limewafukuza watu kutoka katika ardhi zao, limemnyang’anya haki zao, na limekalia juu ya matakatifu yao. Watekelezaji wa vitendo hivi hawana haki yoyote katika wanachokifanya. Kwa hivyo, umma huu unahitaji kuungana kwa moyo, akili, na dhamira moja kupigana na maadui zao, ili kumaliza dhulma zao."
Sheikh Mals alisisitiza: "Katika Jumuiya ya Kuimarisha Umoja na Shirikisho la Wanazuoni wa Kiislamu na mashirika mengine yanayofanana, tuna imani thabiti katika umoja. Taasisi hizi zinapaswa kuwakumbusha Waislamu kuhusu hatari kubwa wanazokumbana nazo na kuwaelimisha. Lazima waendelee kushikamana ili waweze kukabiliana na maadui zao."
Maoni yako