Jumapili 15 Februari 2026 - 21:30
Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran ni kwa ajili ya Waislamu wote na hata watu huru duniani

Hawza/ Sheikh Abdallah Al-Daqqaq, Mkurugenzi wa Hawza ya Wabahreini mjini Qom, ameelezea ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu kuwa ni “mlipuko wa nuru”, huku akisisitiza kuwa; haukuishia ndani ya mipaka ya Iran pekee, bali ni wa Waislamu wote na watu wote wanaopenda uhuru duniani.

Kwa mujibu wa Idara ya Kimataifa ya Shirika la Habari la Hawza, Hujjatul-Islam wal-Muslimin Sheikh Abdallah Al-Daqqaq, Mkurugenzi wa Hawza ya Wabahreini mjini Qom, katika ujumbe wa video alioutoa kutokana na mnasaba wa maadhimisho ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, amelitaja tukio hilo la kihistoria kuwa limebeba ujumbe wa kimataifa kwa mataifa yote huru.

Katika ujumbe wake amesema: “Ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran tarehe 11 Februari mwaka 1979 (22 Bahman), ulikuwa ni sawa na mlipuko wa nuru. Mapinduzi haya hayakuishia Iran pekee; bali ni ya Waislamu wote na hata ya watu wote huru duniani.”

Mwanazuoni huyo wa Kibahreini huku akisisitiza mafundisho ya kudumu ya Mapinduzi ya Kiislamu ameongeza: “Ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran katika siku hii, yaani 22 Bahman / 11 Februari, umebeba ujumbe wa kimataifa; kwamba mataifa hayatapata uhuru kamwe isipokuwa pale yatakapojitokeza yenyewe kwa harakati, na yanapoanza harakati hizo, yanapaswa kubaki imara na thabiti.”

Sheikh Abdallah Al-Daqqaq alihitimisha kwa kusema: “Siku ya 22 Bahman pia imebeba ujumbe mwingine; ujumbe unaosema kuwa; Umma wa Kiislamu hauwezi kukata mikono ya maadui wake isipokuwa kwa kusimama kidete na kwa uthabiti mbele ya ubeberu wa kimataifa.”

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha