Jumatatu 5 Januari 2026 - 11:00
Mji wa Ghubairi nchini Lebanon wafanya hafla ya kumbukizi ya shahada ya kamanda Haj Qassim Suleimani

Hawza/ Mji wa Ghubairi uliopo katika mji wa Baabda nchini Lebanon uliadhimisha kumbukumbu ya shahada ya kamanda Shahidi Haj Qassim Suleimani kupitia hafla iliyofanyika karibu na mnara wa kumbukumbu wa Shahidi Suleimani uliopo katika Barabara Kuu ya Imam Khomeini (ra).

Kwa mujibu wa taarifa ya Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, mji wa Ghubairi katika mji wa Baabda nchini Lebanon uliadhimisha kumbukumbu ya shahada ya kamanda Shahidi Haj Qassim Suleimani kupitia hafla iliyofanyika karibu na mnara wa kumbukumbu wa Shahidi Suleimani uliopo katika Barabara Kuu ya Imam Khomeini (ra). Katika hafla hiyo, kwa ajili ya kutoa heshima kwa roho takatifu za mashahidi, washiriki walitoa mashada ya maua.

Katika hafla hii, walihudhuria Taufiq Samadi, Naibu Balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran; Mhandisi Muhammad Dargham, Rais wa Muungano wa Manispaa za Dahiya ya Kusini; Ahmad Al-Khansa, Meya wa Ghubairi; Naibu Meya na wajumbe wa Baraza la Manispaa, pamoja na wawakilishi wa Harakati ya Amal, Hizbullah na Chama cha Kitaifa cha Syria, wawakilishi wa makundi ya Kipalestina, viongozi wa kijamii na kisiasa, na idadi kubwa ya wakazi wa mji huo.

Katika hotuba zilizotolewa kwenye hafla hiyo, ilisisitizwa kuwa, damu ya mashahidi itaendelea kuwa nuru inayoangaza njia ya muqawama na heshima, na kuwa chanzo cha msukumo kwa vizazi katika safari ya uthabiti na kusimama imara.

Wahutubu walisisitiza juu ya kushikamana na umoja wenye msimamo mbele ya uvamizi na uchokozi, na wakafanya ahadi mpya ya kuendelea na njia iliyochorwa na mashahidi kwa damu yao takatifu, kwa kutimiza uaminifu kwa kujitolea kwao na kulinda maadili ambayo kwa ajili yake walitoa maisha yao kishahidi.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha