Jumanne 6 Januari 2026 - 13:40
Serikali ioneshe ustahiki wake wa kitaifa

Hawza/ Mufti Mkuu wa Jaafaria wa Lebanon alisema: Tupo katika wakati wa machafuko ya kimataifa yanayoongozwa na Washington, huku Ulaya ikisalimu amri, jambo ambalo linaupeleka Umoja wa Mataifa kwenye mwisho wenye kusikitisha sana.

Kwa mujibu wa ripoti ya Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Hujjatul-Islam Sheikh Ahmad Qabalan, Mufti Mkuu wa Jaafaria na kiongozi wa kidini wa Kishia Lebanon, alisema: Tupo katika wakati wa machafuko ya kimataifa yanayoongozwa na Washington, huku Ulaya ikisalimu amri, na hali hii inaupeleka Umoja wa Mataifa kwenye kiini cha mwisho wenye huzuni. Hata hivyo, dunia inabadilika kwa kasi kuelekea mfumo wa kimataifa wa nguvu nyingi, jambo linaleta hatari kubwa zaidi kwenye himaya nzito ya Washington; himaya ambayo hutumia nguvu zake kwa walio dhaifu pekee. Sababu ni kwamba Marekani na Ulaya zinapitia kushindwa kwao kukubwa zaidi nchini Ukraine tangu Vita vya Pili vya Dunia, na mradi wa Washington na Brussels huko unazikwa kwa nguvu. Hatua za Marekani nchini Venezuela ziko karibu zaidi na ndoto potofu kuliko uhalisia, na kupotosha taswira hapa ni jambo muhimu sana; ninamaanisha vita vya “Israel” dhidi ya Iran.

Aliongeza: Vita hivyo [vya Israel dhidi ya Iran] vilikuwa tu kifuniko cha vita hatari zaidi vya kushtukiza vya Atlantiki–Marekani dhidi ya Iran, ambavyo vilimalizika kwa jibu la kuangamiza na kushindwa “Israel” kwa aibu; kushindwa kulikoilazimisha Washington, kupitia upatanishi wa madola muhimu, kutafuta usitishaji mapigano na kuzuia kuangamizwa “Tel Aviv”.

Sheikh Qabalan alibainisha kuwa, muundo wa dunia ya leo ni mgumu zaidi kuliko maonesho ya Kimarekani, na hili ndilo jambo ambalo pande rasmi katika nchi hii [Lebanon] zinapaswa kulielewa, kwa sababu Washington inataka kunufaika na uharamia ambao kupitia kwake ilimteka rais wa Venezuela, Maduro.

Mufti Mkuu wa Jaafaria aliendelea kusema: Kinachohitajika ni uongozi wa Lebanoni wenye ujasiri wa kushughulikia masuala ya kitaifa na ya mamlaka kwa kujiamini kikamilifu na kwa uthabiti. Uongozi wa Lebanon unapaswa kukumbuka kwamba “Israel”, licha ya uungaji mkono mkubwa wa Atlantiki na licha ya vita virefu, vilivyo changamano na vilivyopangwa mapema, ilishindwa kuimarisha nafasi yake katika kijiji chochote cha mstari wa mbele. Hili ni suala la kizalendo; ni suala la nchi yenye nguvu na irada ya ndani inayounga mkono chaguo za kitaifa, na hatupaswi kulipoteza.

Akiashiria kwamba sasa ni wakati wa kuilinda Lebanon dhidi ya michezo ya kupoteza na kutojali, na kwamba uchaguzi unakaribia, alisisitiza kuwa; Lebanon lazima iokolewe kisiasa, na akaomba serikali ya Lebanon ithibitishe ustahiki wake wa kitaifa, kwa sababu kinachotokea katika uwanja wa kisiasa kinaifanya ihesabiwe miongoni mwa wafu.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha