Jumanne 6 Januari 2026 - 15:40
Tuzo ya Kumi na Moja ya Kimataifa ya Arbaeen yatamatika huko Karbala Tukufu

Hawza/ Tuzo ya Kumi na Moja ya Kimataifa ya Arbaeen, kwa kuwatunuku washindi na kusisitiza nafasi kuu ya sanaa na vyombo vya habari katika kusambaza ujumbe wa Ashura duniani, imehitimisha shughuli zake huko Karbala.

Kwa mujibu wa taarifa ya Idara ya Kimataifa ya Shirika la Habari la Hawza, hafla ya kufunga Tuzo ya Kumi na Moja ya Kimataifa ya Arbaeen ilifanyika jioni ya Jumatatu tarehe 5 Jabuary 2026, inayolingana na tarehe 15 Rajab 1447 Hijria Kamaria, katika jengo la Ubalozi Mdogo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mjini Karbala.

Katika hafla hiyo, ambayo ilihudhuriwa na Hujjatul-Islam wal-Muslimin Imani-Pour, Rais wa Shirika la Utamaduni na Mawasiliano ya Kiislamu, pamoja na kundi la maafisa, wanazuoni, wanafalsafa, na wadau wa sanaa na vyombo vya habari kutoka Iraq, Iran na nchi mbalimbali, washindi wa toleo la kumi na moja la Tuzo ya Kimataifa ya Arbaeen walitunukiwa.

Ayatullah Sayyid Mujtaba Husseini, Mwakilishi wa Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iraq, katika hafla hiyo, akitoa rambirambi kutokana na mnasaba wa siku za kufariki dunia kwa Bibi Zaynab (as), alisema:
“Tunapaswa kujifunza kushikamana na Wilaya kutoka kwa Bibi Zaynab (as).”

Aliielezea Tuzo ya Kimataifa ya Arbaeen kuwa ni hatua yenye thamani kubwa katika kuitambulisha Arbaeen kwa watu duniani kwa lugha ya sanaa na vyombo vya habari.

Mwakilishi wa Kiongozi Mkuu, akirejelea mabadiliko ya siku hizi katika uwanja wa dunia, alisema:
“Imam Hussein (as) kwa dhahiri aliuawa kishahidi, lakini katika kufikia lengo lake kuu la harakati ya Ashura alipata ushindi, na matokeo ya ushindi huo ni kwamba hadi leo, jina na ujumbe wa Imam Hussein (as) vinasikika kwenye kila pembe ya dunia. Leo pia mabeberu wa dunia na Wazayuni wanajaribu kuizima sauti ya haki na ukweli, na katika vita vya siku 12 tulipoteza shakhsia kubwa, lakini ushindi ni wetu na mkondo wa Muqawama umeshinda.”

Muhammad Kazem Al-Sadeq, Balozi wa Iran mjini Baghdad, naye pia huku kutoa shukrani kwa waandaaji wa Tuzo ya Kimataifa ya Arbaeen, alirejelea kumbukumbu ya siku ya kuuawa shahidi Haj Qassem Soleimani na Abu Mahdi Al-Muhandis, na akasema:
“Mataifa mawili ya Iran na Iraq yana uhusiano wa kina sana, na kuna mambo mengi ya pamoja ya kitamaduni kati yetu; miongoni mwa nyakati nzuri zaidi za kudhihirisha uhusiano huu ni siku za Arbaeen ya Husseini.”

Nasif Al-Khattabi, Gavana wa Karbala, pia katika hafla hiyo alisema: “Mimi ni mdogo mno kuizungumzia Arbaeen ya Husseini, na ninajiona tu kuwa mtumishi mdogo wa watumishi wa mazuwari wa Sayyid al-Shuhada (as). Hususan Arbaeen, ambayo ni tukio kubwa, la kistaarabu na la kimataifa, halihusiani na Mashia pekee, bali ni nembo ya Uislamu wa kweli na lina ujumbe kwa watu wote huru duniani.”

Jaafar Safari, Kaimu Mkuu wa Ubalozi Mdogo wa Iran mjini Karbala, naye pia kwa kutoa shukrani kwenye mamlaka na taasisi mbalimbali za Iran na Iraq katika kuandaa Tuzo ya Kimataifa ya Arbaeen, alisema:
“Katika hali ambayo vyombo vingi vya habari vya dunia vinafuata sera ya kuficha na kususia maandamano makubwa ya Arbaeen, matukio kama haya ni chanzo cha kheri na yana athari nyingi chanya kwenye jamii ya wasanii na kwa watu duniani ujumla.”

Hujjatul-Islam wal-Muslimin Husseini-Nishabouri, Rais wa Kituo cha Kimataifa cha Tabligh na Katibu wa tukio hili, pia mwanzoni mwa hafla kwa kuwakaribisha wageni wote alisema: “Kazi elfu thelathini na tano (35,000) kutoka nchi 47 duniani zilipokelewa na sekretarieti ya Tuzo ya Kimataifa ya Arbaeen, jambo ambalo lilionesha ongezeko kubwa ikilinganishwa na matoleo ya awali; na tunayaalika makundi yote yanayojitahidi kuifikisha sauti ya Arbaeen kwa walimwengu, kushiriki ili toleo la kumi na mbili la tukio hili lifanyike kwa adhama zaidi.”

Mwisho wa hafla hiyo, bango la toleo la kumi na mbili la Tuzo ya Kimataifa ya Arbaeen lilizinduliwa rasmi.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha