Kwa mujibu wa taarifa ya Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, “Mkutano wa vyama, nguvu na shakhsia za kitaifa za Lebanon” umeilaani hatua ya uvamizi wa wazi wa Marekani dhidi ya serikali ya Venezuela.
Vyama vya Lebanon vimesema katika tamko lao: kwa mara nyingine tena, serikali ya Marekani imeufichua uso wake wa kigaidi na mbaya kupitia uvamizi wake wa jinai dhidi ya serikali rafiki ya Venezuela; uvamizi ambao kwa kiburi na ufidhuli wake umevuka mipaka na kukiuka sheria, kanuni na viwango vyote vya kimataifa, kimaadili na kibinadamu.
Mkutano wa vyama umeeleza kuwa: uvamizi huu unaonyesha kwa uwazi kabisa fikra za ukiritimba na kujiona bora zinazotumiwa na serikali ya Marekani mfululizo katika mahusiano yao na nchi za dunia; fikra ambazo katika kipindi cha rais mpumbavu, Trump, zimezidi hata zile za watangulizi wake wote.
Vyama vya Lebanon viliendelea kubainisha kuwa: uvamizi wa Marekani dhidi ya Venezuela ni tishio kubwa kwa uthabiti na amani ya kimataifa, na ni ukiukaji wa wazi wa mamlaka ya taifa mwanachama wa Umoja wa Mataifa. Zaidi ya hayo, kwa kumteka nyara Rais Maduro na mke wake, uvamizi huo umeweka mfano hatari wa uharamia wa kimataifa.
Mkutano wa vyama ulisisitiza kuwa: uvamizi huu bila shaka ni jinai ya kimataifa inayohitaji hatua ya haraka ya Baraza la Usalama la kimataifa ili kulaani kitendo hiki kichafu, kufanya juhudi za kusitisha mara moja uvamizi huo, na kuhakikisha kuachiliwa huru rais aliyetekwa nyara pamoja na mke wake.
Mkutano huu ulisisitiza tena kwamba: “Mkutano wa vyama, nguvu na shakhsia za kitaifa za Lebanon,” sambamba na kurejea kulaani ugaidi wa Marekani, unaeleza mshikamano wake kamili na wananchi na uongozi wa Venezuela, na hausahau misimamo ya kuunga mkono ya Venezuela kwa mataifa ya Umma wetu, hususan watu wa Palestina na Lebanon, dhidi ya uchokozi wa Kizayuni unaoungwa mkono na Marekani.
Mwisho, mkutano huu uliyaomba mashirika ya kimataifa kutekeleza majukumu yao katika kuzuia dhulma ya Marekani, na ukazihimiza jamii, vyama na nguvu huru duniani kote kueleza wazi chuki yao dhidi ya sera za Marekani ambazo zinakwenda kinyume na haki za binadamu, heshima ya kitaifa na utu wa mwanadamu.
Maoni yako