Kwa mujibu wa taarifa ya Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Rami Abu Hamdan, mjumbe wa kambi ya “Uaminifu kwa Muqawama”, amezilaani kauli chafu zilizotolewa na mbunge wa Lebanon, Bula Ya‘qubian, ambazo zilijumuisha matusi dhidi ya wanazuoni wa dini ya Kiislamu, na akazielezea kuwa ni kuanguka kwa Ya‘qubian hadi katika kiwango cha chini kabisa cha upotovu na ni uvamizi dhidi ya Uislamu pamoja na shakhsia na wakubwa wake.
Abu Hamdan alisema katika tamko lake, akijibu kauli za Ya‘qubian: “Yaliyotoka kwa mbunge Bula Ya‘qubian, yakiwemo matusi machafu dhidi ya wanazuoni wa dini ya Kiislamu na kuwataja baadhi yao wanaohusika katika ulingo wa siasa kwa jina la ‘Shetani Mkubwa’, ni uvamizi wa wazi na wa kihuni dhidi ya dini tukufu ya Uislamu, Mtume Mtukufu (rehema na amani zimshukie yeye na Ahlul-Bayt wake) na Maswahaba wake, na ni matusi hatari sana dhidi ya mfumo wa maadili na misingi ya kimaadili. Inaonekana kwamba mbunge huyu, kwa kauli hizi, ameteremka hadi kiwango cha chini kabisa cha upotovu na uvamizi dhidi ya Uislamu na alama zake.”
Alisisitiza kuwa maneno haya ya aibu na yapo kinyume na Katiba pamoja na sheria zinazotumika ambazo hulinda dini na kupiga marufuku aina yoyote ya uvamizi au uchochezi dhidi yake, na pia yanakinzana waziwazi na maadili ya kuishi kwa pamoja, heshima kwa dini na alama za kidini.
Mjumbe huyo wa kambi ya Muqawama alihitimisha kwa kusema: “Kwa msingi huo, mwenendo huu uliojitenga na mipaka na maadili yoyote hauwezi kuchukuliwa kama maoni ya kawaida au ya kupita tu; bali unalazimisha kuwekwa mpaka wa kisheria ulio wazi na madhubuti, na unahitaji kuchukuliwa hatua na taasisi husika ndani ya mfumo wa Katiba.”
Maoni yako