Jumapili 7 Septemba 2025 - 07:40
Ammar Hakim: Iran ni ngome iliyopo mstari wa mbele katika ulimwengu wa Kiislamu

Hawza/ Kiongozi wa Harakati ya Hikmat ya Kitaifa ya Iraq, alipo hudhuria katika Haram Tukufu ya Imam Khomeini (r.a), alimpa heshima mwanzilishi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Hawza kutoka Tehran, Hujjatul-Islam wal-Muslimin Sayyid Ammar Hakim, kiongozi wa Harakati ya Hekmat ya Kitaifa ya Iraq, alihudhuria katika Haram Tukufu ya Imam Khomeini (r.a) na kutoa heshima zake kwa mwanzilishi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Katika ziara hiyo, Ammar Hakim alielezea umoja na mshikamano Waislamu wote – wa Kishia na Kisunni – na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika vita vya siku 12 vilivyopita na akasema:
“Waislamu, kwa sababu ya chuki yao dhidi ya utawala wa Kizayuni, wanaiunga mkono nchi yoyote inayojihami na kupambana na Israeli.”

Akaongeza kuwa: “Vita vya karibuni vimeleta umoja ndani ya Iran na vimefuta shutuma za zamani za madhehebu dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu katika ulimwengu wa Kiislamu.”

Hakim, akibainisha kwamba Iran haraka ilitoka kwenye mshituko wa shambulio la utawala wa Kizayuni, alitaja pigo kubwa lililopelekwa kwenye ulinzi wa anga wa utawala huo na mshangao wake kutokana na nguvu za makombora ya Iran, Akasisitiza: “Sasa, baada ya kushindwa katika nyanja hii, wao wanatafuta kuleta machafuko ndani ya Iran.”

Mwisho, kiongozi wa Harakati ya Hekmat ya Kitaifa ya Iraq alisema kuwa, Iran ni ngome ya mstari wa mbele katika ulimwengu wa Kiislamu, na akaongeza kwa kusema:
“Leo, nchi za eneo hili zimetambua kuwa iwapo Iran itadhoofishwa katika mapambano yake na utawala wa Kizayuni, basi eneo lote litaathirika na kupata hasara.”

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha