Alhamisi 7 Agosti 2025 - 06:32
Mwandishi wa Hawza: Ukimya wa watawala wa Kiislamu mbele ya njaa inayo wakabili watu wa Ghaza haufahamiki

Hawza/ Mtafiti wa kielimu wa Hawza ametaja kimya cha sasa cha jumuiya za Kiislamu na wanaharakati wa kiraia, kuwa ni miongoni mwa majibu ya kusikitisha zaidi ya Waislamu dhidi ya maadui katili zaidi wa Uislamu.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Hujjat al-Islam wal-Muslimin Hujjatullah Sarwari, katika mahojiano na shirika la habari la Hawza, akirejea kwenye jinai za utawala wa Kizayuni huko Ghaza, amesema: mauaji ya kimbari na jinai za kivita huko Ghaza ni aina ya jinai dhidi ya ubinadamu.

Ameongeza kuwa: janga la njaa lisilo na mfano huko Ghaza, ambalo limechochewa na ushirikiano wa Marekani mhalifu na utawala bandia wa Kizayuni, pamoja na kuendelea uvunjaji wa haki za binadamu kutoka kwao huko Ghaza, linaweza kutajwa kama janga la kibinadamu la kutisha zaidi.

Akiashiria kwamba uvunjaji wa wazi wa haki za binadamu kutoka kwa utawala wa Israel una historia ya urefu sawa na kuanzishwa kwa utawala huo bandia, amesema wazi: kwa mujibu wa takwimu za UNICEF, zaidi ya watu 470,000 huko Ghaza wanakabiliwa na njaa kali, na kati ya kila watu watatu katika Ukanda wa Ghaza, mtu mmoja anapita siku bila kula, na wanahangaika katika kiwango cha chini kabisa cha hatua tano za usalama wa chakula. Wakati huo huo, Shirika la Chakula Duniani katika ripoti yake linasisitiza kwamba watoto 71 wa Ghaza wanahitaji matibabu ya haraka ya utapiamlo, idadi hii ni pamoja na wanawake 17,000 waishio Ghaza ambao wanateseka kutokana na tatizo hilo hilo.

Ameeleza: watu wasio na ulinzi na wasio na hatia, ambao karibu miaka miwili sasa wanabombwa, wanauawa na kujeruhiwa, nyumba zao zinabomolewa, watoto wengi wamekuwa yatima, mama wengi wamepoteza watoto, familia zimefutika na hakuna aliyebaki hai, wamepitia maradhi, kukosa usingizi, njaa na kiu mfululizo, wamepiga kelele kwa majonzi makali na kuomba msaada lakini hawajapata pa kufikia, na bado wamo katika mzingiro huku wakisimama imara kwa kumtegemea Mwenyezi Mungu Mtukufu pekee.

Mwandishi huyu wa Hawza amekumbusha: licha ya sensa zote za habari, leo watu duniani wanaona ni jinsi gani utawala bandia na mhalifu wa Kizayuni unavyowaweka watu wanyonge na wasio na ulinzi wa Ghaza katika mzingiro wa kiu na njaa ya muda mrefu kwa ukatili na ukosefu wa huruma kabisa, huku nchi za Kiislamu zikiwa katika kimya cha kifo.

Ameongeza kuwa: nyote ni mashahidi kwamba, katika siku hizi ngumu na za kifo, watu wa Ghaza waliopoteza wapendwa waliokumbwa na maafa amabo wanauawa mauaji ya kimbari kutokana na mashambulizi ya kijeshi, na pia wanakufa kishahidi kwa sababu ya njaa kali na kiu.

Hujjat al-Islam wal-Muslimin Sarwari amesema: kwa sasa zaidi ya watu 71,000 wanakabiliwa na hatari ya kifo kinachosababishwa na njaa na wanahitaji kufikishiwa haraka dawa na chakula ili kutibu utapiamlo wao mkali. Moja ya jinai za utawala wa Kizayuni, kwa desturi yake, ni kushambulia vituo vya usambazaji wa vyakula huko Ghaza.

Akizihutubia serikali za Kiislamu na wanaharakati Waislamu wote duniani, amesema: kama leo Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) angeuliza ulimwengu wa Kiislamu na Waislamu bilioni mbili, “mmefanya nini mbele ya jinai za Israel huko Ghaza ili kuwalinda na kuwatetea wanaume, wanawake na watoto wa Ghaza waliokumbwa na vita?” Wana jibu gani la kutoa? Na kama leo Nabii Isa angeuliza Wakristo zaidi ya bilioni tatu, “mmefanya nini na msaada gani mmeutoa kwa ajili ya vilio vya mama waliopoteza watoto na baba walifungwa mikono nyuma wakijitetea kwa familia na watoto wao?” Dunia ya Ukristo itajibu nini?

Mtafiti huyu wa Hawza amesisitiza: swali lazima liulizwe kwamba, mbali na dini na madhehebu, enyi wanadamu huru wa dunia mlio na dhamira safi na ya kupenda haki, kwa nini mnatazama jinai nyingi za kikatili na zisizo na utu za Wazayuni wauaji wa watoto dhidi ya watu walioko mikono mitupu na katika mzingiro na hamchukui hatua yoyote?

Hujjat al-Islam wal-Muslimin Sarwari amekumbusha: leo kila mtu anaona watoto wanaokwenda kwa matumaini ya kupata chakula kidogo na kusimama foleni, wanauawa kwa ukatili na ukosefu wa huruma na wanyama wakali wa Kizayuni.

Amesema: leo kila mtu anaona watoto wanaofia mikononi mwa mama zao kutokana na njaa na kiu; kutokana na jinai zisizo na mipaka za utawala wa Israel, watu wa Gaza wanakabiliwa na kifo cha taratibu. Mwenyezi Mungu katika Qur'an anasema kuhusu ugumu wa mioyo ya Mayahudi wa Bani Israel:


«ثُمَّ قَسَتْ قُلُوبُكُمْ مِنْ بَعْدِ ذَٰلِكَ فَهِيَ كَالْحِجَارَةِ أَوْ أَشَدُّ قَسْوَةً ...»

Jinai hizi zinatoka tu katika mioyo migumu na yenye mawe ya Wazayuni.

Mwandishi huyu wa Hawza amesema: Qur'an kwa mtazamo wa jumla inawatambulisha watu hawa kuwa ni maadui wakali zaidi, inasema:


«لَتَجِدَنَّ أَشَدَّ النَّاسِ عَداوَةً لِلَّذِينَ آمَنُوا الْيَهُودَ وَالَّذِينَ أَشْرَكُوا»

“Hakika utawakuta watu wenye uadui mkali zaidi kwa wale walioamini kuwa ni Mayahudi na washirikina.”

Mwenyezi Mungu katika aya ya 64 ya Surah Al-Maida anawataja Mayahudi wa Bani Israel kama watu waasi, wenye kiburi, wafisadi, wachochezi wa vita, waanzishaji wa moto, wauaji, wakatili, wavunjaji wa ahadi, makafiri na wanyonge, na anasema kazi yao ni kuua manabii na kuasi amri za Mwenyezi Mungu.

Amesema: Hakika, katika siku zijazo, nchi za Kiislamu ambazo hazijasimama wala kupambana dhidi ya dhulma na jinai za Wazayuni, katika macho ya vizazi vyote vya kesho, zitabakia daima katika historia wakiwa wamejaa aibu na fedheha.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha