Kwa mujibu wa kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, jijini Sydney wakati wito wa mkutano wa wanaoiunga mkono Palestina ulipotolewa, watu walidhani kwamba ni wachache tu wenye ujasiri ambao wangejitokeza kuishinikiza serikali na kuilazimisha Israel kuachana na mauaji ya kimbari na umwagaji damu, hata hivyo, uwepo mkubwa wa wanaoiunga mkono Palestina ulibadilisha makadirio yote.
Polisi wa New South Wales, walitangaza kwamba makadirio ya awali ya idadi ya umati huo yalikuwa watu 90,000. Lakini msemaji wa waandaaji wa mkutano huo alisema kuwa polisi waliwajulisha kwamba karibu watu 100,000 walihudhuria – hata hivyo, kundi lety kwa kutumia takwimu za uwanja limekadiria kwamba idadi hiyo ilikuwa karibu na watu 300,000.
Baada ya mkutano huu mkubwa na maandamano haya, naibu mkuu wa polisi na msaidizi wake walitangaza kuwa hayo ndio yalikuwa maandamano makubwa zaidi waliyoyashuhudia maishani mwao, na katika kipindi cha miaka 35 iliyopita Sydney haijawahi kushuhudia tukio kama hilo!
Kwa mujibu wa tamko la Makumbusho ya Taifa ya Australia, zaidi ya watu 250,000 walipita juu ya daraja hilo kwa mtiririko endelevu na mfululizo, hali ambayo ilichukua takriban masaa sita kukamilika.
Bob Carr, waziri mkuu wa zamani, alipoulizwa jinsi gani umati unakadirika, alijibu: “Kinachojalisha ni kwamba tumepata fursa kubwa, kwa kushirikiana na polisi wa Sydney na wananchi wote wenye hamasa ambao wameogopeshwa na mauaji ya Israel na walitaka kufanya jambo la kukabiliana nalo.”
Chanzo: The Guardian
Maoni yako