Alhamisi 7 Agosti 2025 - 06:18
Israeli Yakiri Kwamba: “Watu Wote Wanaikhtalifiana na Sisi”

Hawza/ Katika kukiri kusiko na kifani, maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje wa utawala wa Kizayuni wametangaza kupungua kwa kiwango kikubwa cha wafuasi wa utawala huo katika uwanja wa kimataifa, kukiri huku kunatokana na upweke usio na mfano wa utawala huu katika vyombo vya habari.

Kwa mujibu wa kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, kwa mujibu wa ripoti za gazeti la Kiebrania "Yedioth Ahronoth", Wizara ya Mambo ya Nje ya utawala wa Kizayuni imekiri kwamba hadi sasa, na tangia kuanzishwa kwa utawala huu wa jinai, hali ya upweke kama huu kuhusu Israeli haijawahi kuwepo katika vyombo vya habari.

Utawala huu ukiachilia mbali kuwa muundo wetu wa kidiplomasia, umefikia kiwango ambacho hatuwezi tena kuzuia wimbi la kimataifa la ufichuaji dhidi ya Israeli na kulidhibiti.

Wizara hii imesema kwa uwazi kwamba kwa hakika inahisiwa kana kwamba balozi zetu kote duniani zimesalimu amri.

Kwa mujibu wa waangalizi wa kimataifa, nafasi dhaifu ya Israeli katika vyombo vya habari vya kimataifa imezidi, hasa baada ya mauaji ya kikatili na mlvizuizi kwa watu wasio na ulinzi wa Ghaza.

Kusambaa kwa picha za kutisha, ripoti za kina na habari za moja kwa moja kuhusu mashambulizi ya anga ya Israeli dhidi ya Ghaza, kumesababisha kuibuka kwa wimbi kubwa la kuhukumiwa kimataifa, na kuiweka Israeli katika nafasi ya kukhalifu haki za binadamu.

Katika muktadha huu, vituo vinne vya habari vya kimataifa viliandaa tamko dhidi ya vitendo vya Israeli, katika tamko hilo la pamoja, hali ya kusikitisha ya waandishi wa habari huru katika Ukanda wa Ghaza ilichunguzwa, na vyombo hivi vya habari vilieleza:
“Waandishi wetu hawawezi kujipatia mahitaji yao ya msingi, wamekuwa macho na masikio ya dunia huko Ghaza kwa miezi kadhaa.”

Chanzo: Ava Press

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha