Jumanne 5 Agosti 2025 - 23:10
Ayatullah Arafi, amjulia hali Ayatullah Huseini Shahrudi

Hawza/ Mkurugenzi wa Hawza Irani amemjulia hali Ayatullah Sayyid Abdulhadi Huseini Shahrudi, mwakilishi wa zamani wa watu wa mkoa wa Golestan Irani, katika Baraza la Wataalamu wa Uongozi.

Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Hawza, Ayatullah Alireza Arafi, Mkurugenzi wa Hawza nchini Irani, kwa kuhudhuria nyumbani kwa Ayatullah Sayyid Abdulhadi Huseini Shahrudi, mwakilishi wa zamani wa watu wa mkoa wa Golestan nchini Irani katika Baraza la Wataalamu wa Uongozi, alimjulia hali mwalimu huyu mkongwe wa Hawza.

Mkurugenzi wa Hawza katika ziara hii aliulizia hali ya jumla na maendeleo ya matibabu ya Ayatullah Huseini Shahrudi na kumuombea afya njema ili apone kamili.

Ayatullah Huseini Shahrudi naye alitoa shukrani na pongezi kwa uwepo wa Ayatullah Arafi na kwa uangalizi maalumu kwa walimu na wakongwe wa Hawza.

Mwakilishi wa zamani wa watu wa mkoa wa Golestan nchini Irani katika Baraza la Wataalamu wa Uongozi, muda mfupi uliopita alipata majeraha ya uti wa mgongo na kwa sasa anapitia kipindi cha matibabu.

Mwisho wa ujumbe.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha