Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, tarehe 14 Novemba 2000, Gianni Agnelli (baba yake Eduardo) alisaini hati iliyompa mwanawe Eduardo asilimia 25 ya hisa za kampuni ya “Dicembre”, ambayo ndiyo mfuko mkuu wa kifamilia wa Agnelli. Lakini siku moja tu baadaye, mwili wa Eduardo ulipatikana chini ya daraja la barabara kuu ya Turin–Savona. Tukio hilo lilitangazwa rasmi kama “kujinyonga,” lakini sasa nyaraka zilizokamatwa na ofisi ya mwendesha mashtaka wa Turin zinaonesha kwamba Eduardo ndiye alikuwa mrithi halisi, na kwamba kifo chake kilipangwa kwa makusudi ili kuhamisha mamlaka kwa mjukuu wa Gianni Agnelli, yaani John Elkann, Myahudi wa Kizayuni.
Waraka huo unaendana na wosia wa siri wa mwaka 1998, na unakataa simulizi maarufu ya “Barua ya Monaco” ya mwaka 1996 ambayo ilikuwa inamfaidisha Elkann. Nyaraka hizi zilipatikana katika ofisi ya mwanasheria Franco Grande Stevens, mmoja wa wapangaji wa mpango wa kuhamisha madaraka. Hatimaye, sehemu ya urithi ambayo ilipaswa kuwa ya Eduardo ilihamishiwa kwa John Elkann, ambaye leo ndiye rais wa kampuni kubwa ya magari Stellantis.
Mama yake Eduardo, Margarita Agnelli, amepeleka kesi mahakamani akitaka mkataba wa urithi ubatilishwe, huku mawakili wake wakisisitiza kwamba uamuzi huo ulifanyika bila kujua nia halisi ya Gianni Agnelli wala ukubwa wa mali zake. Nyaraka zilizokamatwa zinaonyesha kwamba mpango kamili wa kumpa Eduardo urithi huo ulikuwa tayari, lakini ulisimamishwa kwa sababu ya kifo chake cha ghafla.
Shahidi Eduardo Agnelli alikuwa mtu mwenye hekima, roho ya imani, na Muislamu wa kweli aliyesilimu katika Ushia wa Ithna‘ashariyya, na alikuwa na mapenzi makubwa kwa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran. Imani yake kwa Ahlul-Bayt (a.s.) na mtazamo wake wa kupinga ulimwengu wa kimaada vilipingana moja kwa moja na muundo wa nguvu za kiuchumi za Magharibi. Leo hii, shahada yake inaonekana wazi kuwa ni mauaji yaliyolenga kumwondoa mrithi wa kiitikadi na wa kiroho.
Baada ya kupita robo karne, ukweli umeanza kufichuka tena, na kwa hilo, pazia la uongo na fitna lililopangwa kwa ustadi limeondolewa. Eduardo Agnelli hakuwa mwathirika wa kujiua, bali shahidi wa njia ya haki, ukweli, na madhhabu ya Ahlul-Bayt (a.s.).
Leo, jukumu kubwa limewekwa mabegani mwa wapenda haki duniani kote — kulinda kumbukumbu na njia ya shahidi huyu mwenye kudhulumiwa, na kupambana na upotoshaji wa ukweli.
Maoni yako