Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, marehemu Mwalimu Alama Misbah Yazdi katika mojawapo ya mihadhara ya maadili alizungumzia mada ya «Wadhifa wa binadamu katika mitihani ya Mungu» ambayo tunaiwasilisha kama ifuatavyo:
Sunnah ya Mwenyezi Mungu ni mitihani, na kila siku mitihani hii itakuwa migumu zaidi; kwa hivyo tunapaswa kutegemea mitihani migumu zaidi, je! Katika hali kama hii, wadhifa wa kila mmoja wetu ni upi?
Hali tofauti za kijamii huleta majukumu kwa jamii ambayo hatimaye hubadilika kuwa majukumu ya mtu binafsi, kwa sababu jamii haina kuwepo kwa kujitegemea bila watu wake.
Kwa hivyo, kila mtihani au jukumu linalotokea kwa jamii ni mtihani na jukumu kwa watu wa jamii hiyo.
Kwa kuzingatia kwamba watu wanaelewa, wanatambua, wana imani katika ngazi tofauti, hali ya kijamii na rasilimali tofauti, kila mtu ana wajibu wake maalum.
1. Kujifunza kutokana na yaliyopita na kuimarisha nguvu
Hakika, mazito haya na matatizo yatatokea tena katika siku zijazo, na tunapaswa kutumia uzoefu wa zamani kwa ajili ya maisha yajayo, tunapaswa kutambua na kurekebisha mapungufu yetu na kuimarisha nguvu zetu.
Uzoefu wa mabadiliko haya makubwa ni kwamba hali za jamii hubadilika sana kiasi kwamba hata waumini wa hali ya juu huweza kukumbwa na kukata tamaa.
Qur’ani Tukufu inasema:
«حَتَّی إِذَا اسْتَیْأَسَ الرُّسُلُ وَظَنُّواْ أَنَّهُمْ قَدْ کُذِبُواْ»(Mpaka wakati Mitume walipo kata tamaa na watu walidhani kwamba wamekuwa waongo)
[Yusuf, 110].
Aidha, katika aya nyingine ikimsemesha Mtume (s.a.w) na wafuasi wake imesema:
«أَمْ حَسِبْتُمْ أَن تَدْخُلُواْ الْجَنَّةَ وَلَمَّا یَأْتِکُم مَّثَلُ الَّذِینَ خَلَوْاْ مِن قَبْلِکُم مَّسَّتْهُمُ الْبَأْسَاء وَالضَّرَّاء وَزُلْزِلُواْ حَتَّی یَقُولَ الرَّسُولُ وَالَّذِینَ آمَنُواْ مَعَهُ مَتَی نَصْرُ اللّهِ»(Mnadhani kuwa mtaingia Peponi, bila ya kukujieni kama yaliyo wajia wale walio pita kabla yenu? Iliwapata shida na madhara na wakatikiswa hata Mtume na walio amini pamoja naye wakasema: Lini nusura ya Mwenyezi Mungu itakuja? Jueni kuwa nusura ya Mwenyezi Mungu ipo karibu.)
[Al-Baqara, 214].
Aya hii inaonyesha kwamba si kwamba kwa kuamini tu kazi itamalizika; mziti yote yaliyoikumba jamii ya zamani yatawakumba nyinyi pia, mpaka mtakapohoji, "Basi, lini msaada wa Mungu utatufikia?" Na wakati huo, inasema:
«أَلا إِنَّ نَصْرَ اللّهِ قَرِیبٌ»(Msaada wa Mwenyezi Mungu upo karibu)
[Al-Baqara, 214].
Sisi pia tunapaswa kuwa makini kwamba mitihani na matatizi yatakayotokea mbele yetu yatatufikisha kwenye hali kama hizo; hali itabadilika sana hadi tutapaza sauti:
مَتَی نَصْرُ اللّهِ؟(Lini msaada wa Mungu utatufikia?).
Wakati tumepoteza matumaini yote na tumeacha kumtegemea mtu yeyote isipokuwa Mungu, na hatukuzitegemea nguvu zetu, akili zetu, fedha zetu, au uwezo wetu, basi Mungu anasema:
«أَلا إِنَّ نَصْرَ اللّهِ قَرِیبٌ»(Hakika msaada wa Mwenyezi Mungu uko karibu).
2. Kuwa na imani kamili kwa Mungu ni chanzo cha ushindi
Wale wanaoweza kuanza kujifunza kuto tegemea mtu mwingine isipokuwa Mungu, kwao kila mara
إِنَّ نَصْرَ اللّهِ قَرِیبٌ(Msaada wa Mwenyezi Mungu uko karibu) utakuwa kweli.
Tatizo letu ni udhaifu katika “imani, maarifa na kumuamini Mungu.” Tunasema kwa mdomo kwamba riziki yetu iko mikononi mwa Mungu, lakini moyoni tunadhani lazima tuhifadhi pesa kwa ajili ya siku za usoni! Basi Mungu yuko wapi?!
Tunapaswa kujaribu kuwa katika hali yoyote kwamba hatumtegemei mtu yeyote isipokuwa Mwenyezi Mungu.
Hakika Mungu ametuweka wajibu wa kufanya kazi kwa bidii usiku na mchana, lakini hatupaswi kusahau kwamba Mungu anasema wakati waumini walipokata tamaa, aliwatuma malaika kuwasaidia.
Lakini tusidhani kwamba malaika ndio wanawashinda waumini; bali
«وَمَا جَعَلَهُ اللّهُ إِلاَّ بُشْرَی لَکُمْ وَلِتَطْمَئِنَّ قُلُوبُکُم»(Malaika ni habari njema na faraja kwa mioyo yenu)
[Aali Imran, 126].
Maana ni kwamba malaika walitumwa ili muwe na amani, na inafuatia kusema:
«وَمَا النَّصْرُ إِلاَّ مِنْ عِندِ اللّهِ الْعَزِیزِ الْحَکِیمِ»(Ushindi ni kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mwenye Nguvu na Hikima)[Aali Imran, 126].
Chanzo: Hotuba za marehemu Alama Misbah Yazdi, 1390/12
Maoni yako