Jumatatu 4 Agosti 2025 - 08:33
Taasisi za kidini zaratibu matibabu ya macho nchini Tanzania

Hawza/ Jumuiya ya Shia ya Khoja kwa kushirikiana na Taasisi ya Almustafa pamoja na baadahi ya Taasisi za kidini nchini Tanzania, imeratibu matibabu ya macho kwa wananchi, huku mwitikio wa wananchi ukiwa ni mkubwa kuliko ilivyo tarajiwa

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Baadhi ya Taasisi za kidini nchini Tanzania zimeratibu utoaji wa huduma ya macho kwa raia wa nchi hiyo, zoezi hilo ambalo imekuwa ni ada likifanyika kila mwaka katika viwanja vya Mnazi Mmoja, mwaka huu pia limefanikiwa kufanyika kuanzia tareh 01/ 08/ 2025 hadi tareh 03/ 08 / 2025, ambapo madaktari bingwa wa macho waliweza kutoa huduma kwa wananchi.
Katika zoezi hilo taasisi ya Almustafa nayo pia haikuwa nyuma katika kuonesha na kutoa mchango wake kwa raia katika kuendesha zoezi hilo, vile vile katika kilele cha zoezi hilo Sheikh mkuu wa Jumuiya ya shia ithnaasharia Tanzania (TIC) nae pia alihudhuria, akiambatana na ugeni wake maalumu.

Taasisi za kidini zaratibu matibabu ya macho nchini Tanzania

Baadhi ya wananchi walio hudhuria kwenye tukio hilo

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha