Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, vyombo vya habari vya Brazil vimeripoti kuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo, Mauro Vieira, katika mahojiano aliyoyafanya nao, amesema kuwa kwa sasa Brazil inafanya jitihada za kutekeleza hatua za kisheria na kiutawala ili kujiunga rasmi na kesi ya malalamiko iliyo wasilishwa na Afrika Kusini dhidi ya uhalifu wa Israel.
Aidha, amesisitiza kuwa kwa miezi kadhaa, Brazil imekuwa ikijitahidi kutafuta suluhisho la amani na kufanikisha usitishaji wa mapigano katika vita vya Ghaza, lakini upande wa Israel haukuwa tayari bali kuendelea kuchochea zaidi machafuko.
Kuongezeka kwa unyama huo kumesababisha serikali ya Rais Lula kuchukua msimamo wa kisheria wenye nguvu zaidi kuhusu hatua zake za baadaye dhidi ya Israel.
Ni vyema kutambua kuwa Brazil ni nchi ya sita kutoka Amerika ya Kusini kujiunga na waungaji mkono wa kesi hii, kesi hiyo inatoa wito wa kutumia njia za kisheria na hatua za kimataifa kushughulikia tatizo la vita vya Ghaza na mauaji yasiyo na kikomo yanayofanywa na utawala wa Kizayuni.
Tukio hili linaonesha mwelekeo unaokua wa diplomasia yenye misingi ya maadili miongoni mwa nchi za Amerika ya Kusini.
Maoni yako