Jumanne 15 Julai 2025 - 14:19
Golan Amshutumu Netanyahu kwa Kuzuia Mazungumzo ya Usitishaji Vita Ghaza

Hawza/ Yair Golan, kiongozi wa chama cha Demokrasia cha Israel, amemshutumu Benjamin Netanyahu kwa kuweka vikwazo katika usitishaji wa vita na mazungumzo Ghaza kuhusiana na ubadilishanaji wa wafungwa.

Kwa mujibu wa ripoti ya Kitengo cha tarjuma cha Shirika la Habari la Hawza, Golan, kiongozi wa chama cha Demokrasia cha utawala wa Kizayuni, alijibu ripoti ya New York Times akisema: “Netanyahu katika kipindi chote cha mazungumzo, alikuwa akijali tu kulinda muungano wake wa kisiasa, si uhuru wa wafungwa!”

Aliongeza kwa kusema: “Kwa hakika, ripoti za "New York Times" zinathibitisha kile ambacho kila mtu anakijua. Netanyahu, Smotrich na Ben Gvir wanajishughulisha tu na kuhifadhi nafasi zao za kisiasa, na hawajali hata kidogo kama wafungwa wanaachiliwa au la, au kwamba kwa vitendo vyao, wanaiangamiza Israel!”

Golan alisema: “Iwapo sisi Waisraeli tunataka kuilinda nchi yetu, basi serikali ya sasa ya Israel ni lazima iondoke.”

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha