Jumatatu 14 Julai 2025 - 13:52
Karbala ni ufunuo wa milele wa ukweli katika kioo cha fasihi na utu

Hawza/ Hujjat al-Islam Sayyid Abbas B'aqeri, katika hotuba yake, akiwa amesisitiza nafasi isiyoweza kulinganishwa ya Ashura katika dhamiri ya kibinadamu na historia ya fasihi, amesema kuwa Karbala si tukio la kidini pekee, bali ni ukweli hai na wa kimataifa ambao katika nyakati zote, huwahamasisha watu huru kusimama dhidi ya dhulma.

Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha tarjuma cha Shirika la Habari la Hawza, katika Chuo Kikuu cha Chaudhary Charan Singh kilichoko katika mji wa Meerut, India, kikao kilifanyika huku kikiwa na anuani isemayo “Maana ya kisasa na kifasihi ya tukio la Karbala.” Katika kikao hiki cha kielimu na kitamaduni, kundi la maulamaa, maprofesa wa vyuo vikuu, watafiti, na watu wa fasihi walikusanyika ili kuchunguza vipengele mbalimbali vya tukio la Ashura kwa mtazamo wa kijamii, kifasihi na kibinadamu.

Mzungumzaji mashuhuri kutoka india: Karbala ni ufunuo wa milele wa ukweli katika kioo cha fasihi na utu

Mwanzoni mwa hafla hii, Hujjat al-Islam Sayyid Abbas B'aqeri, Mkurugenzi wa Hawza Ilmiyya ya Hazrat Ghufran Ma'ab, katika hotuba yake alisema:

Karbala ni uwanja ambao Imam Husein (as) akiwa pamoja na wafuasi wake 72 waaminifu, kama vile Mtume wa Uislamu (saww), walisimama dhidi ya jeshi la batili na wakaichagua njia ya haki. Mtukufu huyo alitufundisha kwamba heshima ya binadamu iko juu ya tofauti za kidini na kikabila, na kwamba hadhi ya nafsi ni rasilimali kuu ya kila mtu huru.

Akaongeza kwa kusema kuwa:

Tukio la Karbala si tukio la kihistoria tu, bali ni ukweli hai ambao umeakisiwa katika kila tawi la fasihi ya Kifarsi na Kiurdu, ikiwa ni pamoja na "marsia" (tenzi za maombolezo), "ghazal" (mashairi ya mapenzi na hekima), hadithi fupi, visa, riwaya na khutuba.

Katika kuendelea na kikao hicho, Profesa Aslam Jamshidpuri alipokuwa akizungumzia umuhimu wa mikutano kama hii, alisema:

Lengo kuu la kuandaa mikutano ya aina hii ni kujenga uhusiano wa moyo kwa moyo na kupunguza tofauti za kidini na kimtazamo katika jamii. Tukio la Karbala halina kifani katika historia ya mwanadamu; si tu kwamba athari yake haijapungua hata baada ya kupita maelfu ya miaka, bali imezidi kuwa yenye nguvu na kuenea zaidi siku hadi siku.

Akaongeza kuwa: Popote pale dhulma inapojitokeza, jina na kumbukumbu ya Imam Husein (as) kama nembo ya kusimama kidete na uhuru, hufufuka katika nyoyo za watu.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha