Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha tarjama cha SShirika la Habari la Hawza, ongezeko la tuhuma hizo limechochea kampeni kubwa ya kimataifa inayolenga kuishinikiza Abu Dhabi iwajibike kwa kile ambacho wanaharakati wamekieleza kuwa “kuingilia moja kwa moja katika kuchochea migogoro ya kikanda na kufadhili mauaji ya halaiki yanayoendelea mjini Al-Fashir.”
Katika siku za hivi karibuni, alama ya reli (#) “Taharimu Imarat” (Boycott UAE) imekuwa miongoni mwa mitindo (trends) maarufu kwenye mitandao ya kijamii kama sehemu ya kampeni ya kimataifa ya kulaani hatua za UAE.
Wanaharakati wamesema kuwa kinachoendelea si “tofauti za kisera,” bali ni “ufichuzi wa mtazamo unaosambaza vurugu kwa jina la uthabiti na kufadhili vita kwa kivuli cha amani.”
Huko Sudan - hususan katika jiji lililokumbwa na maafa la Al-Fashir — watumiaji wa mitandao wamelinganisha hali ya sasa na “Ghaza nyingine,” wakielezea kuzorota kwa hali ya kibinadamu, pamoja na mtiririko wa silaha na fedha kutoka nje unaoendeleza mapigano kati ya jeshi la Sudan na wanamgambo wa kikosi cha “Al-Da‘am al-Sari‘.”
Tuhuma za Kimataifa na Ushahidi wa Kijasusi
Katika tukio muhimu, gazeti la Wall Street Journal likinukuu maafisa wa ujasusi wa Marekani, limefichua kwamba Umoja wa Falme za Kiarabu katika miezi ya hivi karibuni umekuwa ukituma shehena kubwa za silaha, ikiwemo ndege zisizo na rubani (drones) za kisasa kutoka China, kwa vikosi vya “Al-Da‘am al-Sari‘.”
Gazeti hilo liliripoti kuwa ripoti za Wakala wa Ujasusi wa Ulinzi wa Marekani (DIA) na Ofisi ya Ujasusi ya Wizara ya Mambo ya Nje zinaonesha kuwa tangia majira ya kuchipua mwaka huu, kumekuwa na ongezeko kubwa la vifaa vya kijeshi vinavyotoka UAE kwenda kwa vikosi hivyo, jambo ambalo limezusha hasira kubwa Washington, ambayo imekuwa ikijaribu kudhibiti kuongezeka kwa migogoro nchini Sudan.
Aidha, baadhi ya ripoti zilizotolewa mwezi Oktoba ziliorodhesha aina ya silaha zilizotumwa, zikitegemea picha za uwanjani na taarifa za kijasusi zilizothibitisha kuwapo kwa shehena hizo kutoka UAE, ambazo zilifikishwa mikononi mwa wanamgambo wanaotuhumiwa kwa ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu na mauaji ya raia.
Ripoti za Uingereza na Ushahidi wa Umoja wa Mataifa
Katika muktadha huo huo, gazeti la Uingereza The Guardian lilichapisha ripoti ya uchunguzi iliyoandaliwa na mwandishi Mark Townsend, ambayo ilifichua kwamba silaha na vifaa vya kijeshi vilivyotengenezwa Uingereza vimekutwa mikononi mwa makundi yanayotuhumiwa kutekeleza mauaji ya kimbari nchini Sudan.
Gazeti hilo lilinukuu kesi mbili zilizochunguzwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, ambazo zilionesha wasi wasi makubwa kuhusu mauzo ya silaha za Uingereza kwa UAE, ambayo inatuhumiwa kuzipeleka silaha hizo kwa wanamgambo wa vikosi vya “Al-Da‘am al-Sari‘.”
Gazeti hilo, likimnukuu Mike Lewis, mtaalamu wa Uingereza katika biashara ya silaha, liliainisha kwamba; sheria ya Uingereza inailazimisha serikali kutoidhinisha mauzo ya silaha endapo kuna hatari ya wazi kwamba silaha hizo zinaweza kutumika katika uhalifu wa kimataifa au kupotoshwa matumizi yake.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, mifumo ya kutolea malengo (targeting systems), silaha nyepesi, na injini za magari ya kivita yaliyotengenezwa Uingereza vimekutwa katika uwanja wa vita nchini Sudan, zikitumiwa na vikosi vya msaada wa haraka (Al-Da‘am al-Sari‘) wakati wa mashambulizi yao dhidi ya maeneo ya kiraia — mashambulizi yaliyosababisha mauaji ya halaiki, uhamaji mkubwa wa watu, na kile ambacho Umoja wa Mataifa umekiita “janga kubwa zaidi la kibinadamu duniani.”
Maoni yako