Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha tarjuma cha Shirika la Habari la Hawza Hujjat al-Islam wal-Muslimin Sheikh Ali Najafi, mwana wa Ayatollah al-‘Uzma Hafidh Bashir Husayn Najafi na Mkurugenzi wa Ofisi Kuu ya Marjaa huyo, katika kikao cha maombolezo katika Husayniyya ya Haj Jasem Hanoun huko Karbala al-Mu‘alla, huku akisisitiza upande wa urekebishaji wa harakati ya Imam Husayn (as), amesema kwamba harakati hiyo ni kielelezo cha kudumu kwa ajili ya kuikomboa jamii ya mwanadamu kutoka kwenye upotofu na upoteshwaji.
Akiashiria upeo mpana na kina cha harakati ya Ashura, ameielezea harakati ya Imam Husayn (as) kuwa ni mwamko mkubwa na wa kina wa marekebisho ya kila nyanja, na akasisitiza kuwa Sayyid al-Shuhadā’ (as), kwa kujitolea maisha yake pamoja na watu wa nyumbani kwake na wafuasi wake waaminifu, aliukomboa Ummah wa Kiislamu kutoka kwenye upotovu, dhulma na kupotea njia. Kwa mujibu wa maneno yake, lengo kuu la harakati hii ni kutoa ujumbe wa milele kwa ajili ya kufanya islah (marekebisho) ya mtu binafsi, tabia, mahusiano ya kijamii na uhusiano wa mwanadamu na Mola wake Mtukufu.
Maoni yako