Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, maulamaa wakubwa, mamufi, wanazuoni na viongozi wa nchi za Kiislamu wametoa tamko rasmi la kuwahukumu Donald Trump na Benjamin Netanyahu kwa anuani ya wanaoupiga vita uislamu na waharibifu duniani, tamko hilo ni kama ifuatavyo:
بِسْمِ اللهِ الرَّحْمنِ الرَّحِيمِ
Sifa njema zinamstahiki Mwenyezi Mungu Bwana wa viumbe, na rehema na amani zimshukie Mtukufu wetu Muhammad na Ahlulbayt wake watakatifu, na Maswahaba zake wateule. Ama baada ya yote:
Sisi, maulamaa wakubwa, maftwa, wanazuoni na viongozi wa nchi za Kiislamu, tukitegemea maandiko ya wazi ya Qur’ani Tukufu, Sunna za Mtume (saw), misingi ya wazi ya fiqhi ya Kiislamu na kanuni thabiti za sheria za kimataifa, kwa msimamo madhubuti na kwa kauli moja tunatangaza misimamo ifuatayo:
1. Hukumu ya wazi dhidi ya Trump na Netanyahu kuwahukumu kwa anuani ya wanaoupiga vita uislamu na waharibifu duniani
Kwa mujibu wa Aya Tukufu:
إِنَّمَا جَزَاءُ الَّذِينَ يُحَارِبُونَ اللَّهَ وَرَسُولَهُ وَيَسْعَوْنَ فِي الْأَرْضِ فَسَادًا أَنْ يُقَتَّلُوا أَوْ يُصَلَّبُواBasi malipo ya wale wanao mpiga vita Mwenyezi Mungu na Mtume wake na wakawania kufanya uchafuzi katika nchi, ni kuuwawa, au kusalibiwa...(Al-Māida: 33)
Trump, Netanyahu na viongozi wa utawala wa Kizayuni wanaoikalia kimabavu Quds wanatambuliwa kuwa ni wapiganaji dhidi ya Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, na mafisadi wakubwa katika ardhi, kutokana na kusambaza uharibifu, kumwaga damu, kuyakalia kwa nguvu maeneo ya Kiislamu, kuua kinyama watu wa Palestina na kufanya jinai dhidi ya ubinadamu, wanapaswa kufikishwa mbele ya mahakama za kimataifa na mahakama za Kiislamu ili wachukuliwe hatua.
2. Kuunga mkono uongozi wa hekima na ujasiri wa Ayatollah al-Udhma Imam Khamenei (Mola amuhifadhi)
Ayatollah Khamenei, kama kiongozi wa kuuamsha Umma wa Kiislamu na wabeba bendera walio mstari wa mbele wa izza ya Kiislamu, anaiongoza njia ya heshima, muqawama na umoja wa Waislamu kwa hekima, ujasiri na maarifa. Tunamtambua kuwa ndiye kiongozi halali na anayestahiki kuongoza na kutetea Umma wa Kiislamu.
3. Msisitizo wa kifiqhi, kisheria na kimataifa kuhusu batili ya aina yoyote ya mapatano na Israel na Marekani
Kwa mujibu wa misingi ya wazi ya sheria ya Kiislamu, hasa kanuni ya “kutokufaa kuwa na urafiki au mapatano na makafiri wanaopigana vita dhidi yenu”, na kwa kuzingatia nyaraka za haki za binadamu za kimataifa na haki za mataifa kuamua hatima yao wenyewe – aina yoyote ya mapatano, uanzishaji wa uhusiano wa kawaida au ushirikiano na utawala batili wa Kizayuni unaokalia kwa mabavu ardhi za Kiislamu, pamoja na siasa za kiistikbari za Marekani – ni haramu kisheria, ni usaliti kwa Umma wa Kiislamu, na ni uvunjaji wa wazi wa haki za watu wa Palestina na mataifa yanayodhulumiwa katika eneo hili.
4. Wito wa Umoja wa Kiislamu na wa Wanazuoni mbele ya njama za Kizayuni na mabaradhuli
Leo zaidi ya wakati mwingine wowote, Umma wa Kiislamu unahitaji umoja, mshikamano wa kielimu, kimtazamo, kidini na kisiasa. Sisi maulamaa wa Kiislamu tunawalingana Waislamu wote na wasomi wa ulimwengu wa Kiislamu kushikamana, kuungana katika neno, na kuunda safu ya pamoja dhidi ya njama za Marekani, Israel na washirika wao.
5. Kukiri ushindi kamili wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika vita vya kulazimishwa vya siku 12 na Israel ushindi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika vita vya siku 12 dhidi ya utawala wa Kizayuni ni kielelezo cha nguvu ya imani, muqawama, hekima ya uongozi na uimara wa mstari wa mapambano ya Kiislamu. Ushindi huu haukuwa tu wa kijeshi, bali pia ulileta pigo kubwa kwa mabaradhuli katika nyanja za kisiasa, vyombo vya habari, kisaikolojia na kimataifa, na umethibitisha kuwa zama za utawala usiopingwa wa Marekani na Israel zimefikia kikomo.
6. Wito wa kuhukumiwa kimataifa magaidi na wafuasi wa Kizayuni
Tunatoa wito wa kuundwa haraka kwa mahakama huru za kimataifa ili kuwahukumu Trump, Netanyahu na viongozi wengine wafanya jinai wa Israel pamoja na washirika wao. Tunaziomba taasisi za haki za binadamu, mahakama za kimataifa na mashirika halali ya kisheria kuchunguza jinai hizi dhidi ya ubinadamu na amani ya dunia, na kuchukua hatua za kisheria stahiki dhidi yao.
7. Kufanywa upya kwa bai‘a ya Umma wa Kiislamu kwa lengo la kuikomboa Palestina na Quds Tukufu
Kadhia ya Palestina, Qibla cha kwanza cha Waislamu, yaani Quds Tukufu, bado ni kipaumbele cha juu kwa Umma wa Kiislamu, na hadi kufanikishwa kwa ukombozi kamili wa Palestina na kuangamizwa kabisa kwa donda hatari la Kizayuni, mapambano ya halali na ya kila upande yataendelea bila kusita.
«وَمَا النَّصْرُ إِلَّا مِنْ عِندِ اللَّهِ الْعَزِيزِ الْحَكِيمِ»
Maoni yako