Jumanne 15 Julai 2025 - 14:20
Kuasisiwa Maktaba katika Kila Kituo cha Kiislamu Nchini Maldives Kabla ya Mwisho wa Mwaka Huu

Hawza/ Dkt. Muhammad Shaheem alisema kwamba: Tunakusudia hadi ifikapo mwisho wa mwaka huu wa Miladia, kuasisi angalau maktaba moja katika kila kituo cha Kiislamu nchini Maldives.

Kwa mujibu wa ripoti ya Kitengo cha tarjuma cha Shirika la Habari la Hawza, Dkt. Muhammad Shaheem Ali Said, katika hotuba yake ya sherehe rasmi ya uzinduzi wa maktaba mpya katika Msikiti wa Mfalme Salman nchini Maldives, alisema: Mpango wa “Msikiti Mmoja, Maktaba Moja” umeonyesha mafanikio makubwa, na ni miongoni mwa hatua zilizochukuliwa na Rais wa Jamhuri Dkt. Muhammad Muizzu katika jitihada za kuendeleza maadili ya Kiislamu, na unaonesha upeo mpana wa mtazamo wake kuhusu uenezaji wa elimu za Kiislamu.

Aliongeza kuwa: Serikali, kwa mujibu wa utekelezaji wa mpango huu, ina ratiba mahsusi inayolenga kuhakikisha kuwa mpaka mwisho wa mwaka huu wa Miladia, kila msikiti na kituo cha Kiislamu nchini Maldives kitakuwa na angalau maktaba moja.

Chanzo: Shirika la Habari PMS

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha