Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, kundi la viongozi wa kidini na maafisa wa Baraza la Umoja wa Waislamu wa Pakistan, katika mkutano wa pamoja na waandishi wa habari katika ukumbi wa wanahabari katika jiji la Lahore, Pakistan, walisisitiza juu ya haki ya kisheria ya kuendesha maombolezo, na wakatangaza kuwa hawatakubali kabisa kuwepo kwa aina yoyote ya kizuizi, shinikizo au kikwazo katika njia hiyo.
Viongozi hao, sambamba na kusisitiza kwamba uhuru wa kidini ni haki ya kisheria na ya msingi kwa wafuasi wote wa dini na madhehebu nchini Pakistan, walionya kuwepo mienendo ya kibaguzi na isiyo ya haki dhidi ya waandaaji wa majlisi na washiriki wa sherehe za maombolezo, kwani mienendo hiyo italeta athari mbaya kijamii na kusababisha kuongezeka kwa hisia za kukosekana kwa haki ndani ya jamii.
Maoni yako