Jumatano 2 Julai 2025 - 14:27
Video / Utetezi wa kishujaa wa Seneta wa Pakistan kwa Ayatollah al-Udhma Khamenei

Hawza / Kauli za Hujjatul-Islam wal-Muslimin Raja Nasir Jafari, Mwenyekiti wa Baraza la Umoja wa Waislamu wa Pakistan.

kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Hujjatul-Islam wal-Muslimin Raja Nasir Jafari, Mwenyekiti wa Baraza la Umoja wa Waislamu wa Pakistan amesema kuwa;

Jana, Trump mpumbavu alitishia kwamba atamuua kiongozi na marjaa wetu wa kidini, hili ni sawa na mtu kusema: “Nitamuua Papa.” Ayatollah Khamenei ni kiongozi wetu wa kidini na marjaa wa taqlid wetu, na pia ndiye kiongozi wetu wa kisiasa kwa sababu dini na siasa havitengani. Marjaa wetu ametangaza fatwa kwamba yeyote anayemtishia Kiongozi ni "muharib" (mtu mwenye kuupiga vita uislamu), na hukumu ya muharib katika Uislamu ni kifo.

Trump na Netanyahu wafahamu kwamba endapo shambulio lolote litafanyika, basi hilo halitakuwa shambulio dhidi ya Iran tu, bali jibu la shambulio hilo litatolewa na Waislamu wote wa ulimwengu, sisi hapa Pakistan pia tutatoa jibu, na hawa [maadui] wafahamu kwamba hawatakuwa na nafasi tena Pakistan, ikiwa hatua kama hiyo itachukuliwa, basi hakuna Mmarekani hata mmoja atakayebakia Pakistan.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha