Alhamisi 18 Juni 2026 - 15:18
Maadui wa Iran ni Muendelezo wa Kambi ya “Watu waliopatwa na ghadhabu ya Mwenyezi Mungu” Iliyotajwa katika Qur’ani

Hawza/ Dkt. Abdulhadi Awang, Rais wa Chama cha Kiislamu cha Malaysia, huku akitumia ibara ya “المغضوب عليهم” iliyotajwa katika Suratul-Hamd, amewataja maadui wa leo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuwa ni muendelezo wa kambi ileile ambayo Qur’ani Tukufu imeielezea kuwa ni watu waliopatwa na ghadhabu ya Mwenyezi Mungu, aidha, amemuomba Mwenyezi Mungu awape watu wa Iran ushindi wa wazi mbele ya uvamizi na mzingiro wa kigeni.

Kwa mujibu wa Kitengo cha Kimataifa cha Shirika la Habari la Hawza, Dkt. Abdulhadi Awang, Mwenyekiti wa Chama cha Kiislamu cha Malaysia, katika hotuba yake kwenye mkutano wa kimataifa wenye anuani ya “Watoto Mashahidi, Kushindwa kwa Tawala ya Marekani na Kuamka kwa Umma wa Kiislamu”, ulioandaliwa na Majma‘ ya Kimataifa ya Qadimun na kurushwa kupitia kituo cha televisheni cha Al-Kawthar, alielezea mshikamano wake na wananchi wa Iran, na kumuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu awape watu na viongozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mafanikio, uthabiti na ushindi katika kukabiliana na uvamizi na mashinikizo ya kigeni.

Akiashiria Aya za Qur’ani Tukufu, alisema: “Tunamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu awasaidie Waislamu wa Iran na serikali ya Jamhuri ya Kiislamu mbele ya wale waliopatwa na ghadhabu ya Mwenyezi Mungu; wale ambao Qur’ani Tukufu imewataja kwa ibara ya «المغضوب عليهم», na ambao Waislamu katika swala zao za kila siku humuomba Mwenyezi Mungu awaepushe na njia yao.”

Alisisitiza kuwa; maombi yake ni kwamba: Mwenyezi Mungu awajaalie watu wa Iran ushindi wa wazi na uthabiti katika kukabiliana na changamoto na mashinikizo wanayokabiliana nayo kutoka kwa maadui wao.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha