Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Sayyid Ibrahim Khalil Razavi, Mkurugenzi wa Kituo cha Mafunzo ya Kiislamu cha Khulna na Raisi wa Baraza la Maulamaa wa Imamiyya wa Bangladesh, amevitaja vitisho vinavyo tolewa na utawala wa Kizayuni dhidi ya Marjaa wa Kishia kuwa ni dalili ya kukata tamaa kwa utawala huo, na amevilaani vikali, matini ya tamko hilo ni kama ifuatavyo:
Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu
{ وَقُلۡ جاءَ ٱلحَقُّ وَزَهَقَ ٱلبـطِلُۚ إِنَّ ٱلبَـٰطِلَ كَانَ زَهُوقا}
“Na sema: Haki imefika na batili ikaangamia. Hakika batili huwa linaangamia.” (Al-Isra: 81)
Kwa heshima ya Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu
Mtukufu Ayatollah al-‘Uzma Imam Khamenei (mudda dhilluhu al-‘āli)
Assalamu ‘alaykum wa rahmatullahi wa barakatuh
Ewe mlezi wa mambo ya Waislamu wa dunia, ewe mbeba bendera ya heshima ya Uislamu, ewe faqihi mwenye hekima na marjaa mwenye basira, sisi tukiwa na mioyo iliyojaa imani, mapenzi na yakini thabiti, tunathibitisha na kukiri uongozi wa juu wa kidini, wa kisiasa na wa kiwilaya wa Mtukufu Nyinyi, na tunachukulia utiifu kwa amri zenu tukufu kuwa ni jukumu la kisharia, la kiakili na la kimapinduzi.
Katika zama hizi ambapo kambi ya ukafiri na unafiki, kwa kutumia nguvu zake zote pamoja na vyombo vya habari na kisiasa, inajaribu kudhoofisha nafasi tukufu ya Wilayat Faqih na Marjaa wa Kishia, sisi kwa sauti ya juu tunatangaza:
“Wilayat Faqih ni mstari mwekundu wa Umma wa Kiislamu, na Imam Khamenei ni mbeba bendera ya heshima, uhuru na muqawama wa mataifa yaliyodhulumiwa mbele ya ubeberu wa kimataifa.”
Njama mbaya na za kinafiki za mfumo wa ubeberu na Uzayuni wa kimataifa ambazo kupitia vitisho, vikwazo na operesheni za kisaikolojia zinaibua kudhoofisha nafasi ya uongozi na Marjaa wa Mtukufu wewe, si tu ni dalili ya udhaifu na kukata tamaa kwao, bali pia ni ishara ya athari ya kina ya maneno, misimamo na mwongozo wa hekima wa Waliyat Faqih katika mlingano wa kimataifa.
Sisi tunavilaani vikali vikali vitendo hivi vya kiadui na vya uchochezi, na tunasisitiza kwa msimamo thabiti utiifu wetu kamili kwa njia safi ya Wilaya, na uungaji mkono wetu wa dhati na usio na masharti kwa Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi.
Tunamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu aendelee kuudumisha na kuuimarisha kivuli chako chenye nuru juu ya Umma wa Kiislamu hadi kufika kwa maulana wetu Imam Mahdi (arwāḥunā lahū al-fidā’).
Wassalamu ‘alaykum wa rahmatullahi wa barakatuh
Sayyid Ibrahim Khalil Razavi
Mkurugenzi wa Kituo cha Mafunzo ya Kiislamu, Khulna, Bangladesh
Raisi wa Baraza la Maulamaa wa Imamiyya Bangladesh
Maoni yako