Kwa mujibu wa ripoti ya Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, hatua ya Donald Trump kuandikishwa na kuthibitishwa kama mgombea wa kupokea Tuzo ya Amani ya Nobel na Benjamin Netanyahu, waziri mkuu muhalifu wa Israel, imezua mitazamo mingi duniani kote.
Jozef Borrell, mwanasiasa wa zamani wa Umoja wa Ulaya, aliandika katika akaunti yake ya X kuwa:
“Ni jambo la kushangaza sana kuona kwamba mhalifu (Netanyahu), ambaye hati ya kukamatwa kwake imetolewa na jumuiya ya kimataifa, anamteua mfadhili wake mkubwa wa silaha (Trump) – anayezitumia kwa ajili ya mauwaji ambayo hayajawahi kutokea – kama mgombea wa kupokea Tuzo ya Amani ya Nobel!”
Marekani ndiyo mfadhili mkubwa zaidi wa silaha kwa utawala wa kigaidi wa Israel, na vita vya Ghaza vinaendeshwa kwa msaada kamili wa Ikulu ya Marekani ambayo kila siku hudai kuwa na moyo wa kibinadamu na huruma kwa Wapalestina.
Borrell pia aliandika: “Je, mhalifu wa kivita anajiona kuwa anastahiki kupokea Tuzo ya Amani ya Nobel?!”
Chanzo: Shirika la Habari la Ava
Maoni yako