Jumamosi 28 Juni 2025 - 13:47
Hasira ya Trump kwa sababu ya Muislamu kugombea umeya katika jimbo la New York

Hawza/ Donald Trump alimtaja Zohran Mamdani, ambaye alikuwa mgombea wa umeya katika jimbo la New York, kuwa mmoja wa wafuasi wakuu wa Palestina nchini Marekani, jambo lililotokea huku idadi ya kura ikionesha uwezekano mkubwa wa kushinda kwake.

Kwa mujibu wa ripoti ya Kitengo cha tarjuma cha Shirika la Habari la Hawza, Andrew Cuomo, meya wa zamani wa New York, alishindwa katika uchaguzi wa usiku wa Jumanne, na Zohran Mamdani akachaguliwa kuwa meya wa kwanza Muislamu katika jiji la New York.

Mamdani tangu mwanzo alikuwa ni mfuasi imara wa Palestina na mkosoaji mkali wa Israel pamoja na mashambulizi ya kijeshi na mauaji yanayofanywa na utawala huo.

Mwaka 2020, katika akaunti yake ya X (zamani Twitter), alisema kuwa alianzisha kampeni katika chuo kikuu cha (Alma College) ambako wanafunzi wanaoiunga mkono Palestina walikuwa wakifanya shughuli mbalimbali. Mamdani anaamini kuwa jitihada na kusimama imara kwa wanafunzi wanaoiunga mkono Palestina kunachochea hisia za huruma miongoni mwa watu kwa ndugu zetu wa Kipalestina.

Mnamo mwaka 2023, alijiunga na kambi ya mgomo wa kula iliyokuwa nje ya Ikulu ya Marekani (White House) na alihesabiwa miongoni mwa watu waliokuwa wakidai sitisho la vita (kusitishwa kwa mashambulizi).

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha