Jumamosi 12 Julai 2025 - 00:22
Wanafunzi wa Yemeni waanza mwaka mpya wa masomo kwa maandamano ya kuiunga mkono Ghaza

Hawza/ Wanafunzi wa Yemeni hufanya maandamano kila wiki kwa namna ya kishujaa kulaani kimya cha jumuiya ya kimataifa mbele ya mateso ya watu wa Ghaza.

Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha tarjuma cha Shirika la Habari la Hawza, wanafunzi wa Yemeni na Chuo Kikuu cha Sana’a, wakiwa pamoja na makundi mengine ya watu wa Yemen, huandaa mikusanyiko mikubwa kila wiki ili kulaani jinai zinazofanywa na utawala wa Kizayuni dhidi ya Ghaza.

Maandamano haya hufanyika kwa ushiriki wa wanafunzi wa kiume na wa kike, pamoja na baadhi ya walimu wa vyuo vya ualimu na maafisa wa Chuo Kikuu cha Sana’a. Uwepo mkubwa wa wanafunzi wa kiume na wa kike kwa namna ya pekee katika maandamano haya unaonesha kuwa Wayemeni wameunganisha elimu, imani na utambuzi wa kisiasa, na sifa hizi zimekuwa ngome isiyoweza kuvunjika mbele ya wageni na maadui wa Yemen.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha